TAKUKURU YAMHOJI PAUL CHRISTIAN SAKATA LA VYETI

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Tabora, inamsaka mwandishi na mtangazaji wa Redio Sauti ya Tabora (Voice of Tabora), Paul Pele Christian kwa siku kadhaa sasa bila mafanikio.
Habari za uhakika zilizopatikana mjini Tabora, zinasema kuwa maofisa wa taasisi hiyo wamekuwa wakimsaka kwa mahojiano kuhusu kashfa inayomuhusisha na sakata la vyeti vya elimu anavyodaiwa kuvitumia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kujiendeleza kielimu.
Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Tabora, Fidelis Kalungula alieleza kuwa wanamtafuta Christian kwa siku kadhaa sasa, lakini hawajafanikiwa kumpata.
“Kweli tunamtafuta kwa mahojiano, hatujafanikiwa kuonana naye,” alisema Kalungula bila kufafanua zaidi.
Akizungumza kwa simu , Christian alikiri kupigiwa simu na maofisa wa taasisi hiyo wakimtaka afike ofisini kwao kwa mahojiano.
“Nimepigiwa simu na maofisa wa Takukuru nifike ofisini kwao, leo ni siku tano sijatokea ,” alisema.
Christian alisema kila anapohitajika amekuwa akibanwa na majukumu mengi ya kazi zake, hivyo kushindwa kuwajibu lolote akihofia kuwapotezea muda wao.
Alisema hii si mara ya kwanza kuhojiwa na maofisa wa taasisis hiyo, kwani walishafanya hivyo mara mbili.
Christian alisema mara ya kwanza ilikuwa Aprili 15, mwaka huu aliopigiwa simu na kaimu Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Tabora, akidai ana mazungumzo na yeye.
Baada ya wito huo alifika ofisi za Takukuru saaa 8:20 mchana.
“Katika mazungumzo yetu, walitaka kujua historia ya niliposomea kuanzia elimu ya msingi, sekondari, chuo na ninamfahamu vipi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam” alisema.
Aliongeza kuwa mara ya pili alihojiwa tena Mei 10, mwaka huu saa 5 asubuhi kwa muda wa saa tatu.
“Mbali na mahojiano na maofisa hao, niliwakabidhi nakala za vyeti vyangu vya elimu ya Sekondari,” alisema.
Pia Mei 15, mwaka huu alipata taarifa ya kutafutwa tena na ataasisi hiyo kwa mahojiano kupitia kwa mkurugenzi wake wa Voice of Tabora, Ismail Ade Rage.
Christian alisema kuwa yeye anashangazwa na hatua ya kutafutwa mara kwa mara, japo mhusika wa suala hilo yuko Dar es Salaam.
HT @ MTANZANIA
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post