TIMU YA MANCHESTER CITY YAIFUNGA MKONO CRYSTAL PALACE

Manchester City wamejiimarisha katika kuhakikisha wanamaliza katika nafasi nne za juu za Ligi Kuu ya Uingereza kwa kupata ushindi mnono wa magoli 5-0 dhidi ya Crystal Palace na kukwea juu ya Liverpool hadi katika nafasi ya tatu.

Katika mchezo huo David Silva alifunga goli la kwanza ndani ya dakika mbili tu, likiwa goli lililofungwa mapema mno katika msimu huu, lakini baada ya hapo iliwachukua muda mrefu wenyeji Manchester City kuweza kuutawala mchezo huo.

Kikosi cha Pep Guardiola kilijihakikishia kuondoka na pointi zote tatu katika kipindi cha pili baada ya kapteni Vincent Kompany kufunga kupitia krosi ya Kevin de Bruyne, kisha De Bruyne akifunga la tatu, Raheem Sterling akafunga la nne na Nicolas Otamendi akahitimisha karamu.
                     David Silva akiifungia Manchester City goli la kwanza katika mchezo huo
                                 Kapteni Manchester City Vincent Kompany akifunga goli la pili
                       Raheem Sterling akiachia shuti lililojaa wavunia na kuandika goli la nne
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post