UPDATED: POLISI WATHIBITISHA WANAFUNZI 31 WAFARIKI KATIKA AJALI YA BASI KARATU

TAARIFA ZA AWALI
Wanafunzi zaidi ya 20 wanahofiwa kupoteza maisha katika ajali ya basi iliyotokea wilayani karatu leo asubuhi.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa, basi hilo aina ya Mitsubish Rosa lilikuwa limewabeba wanafunzi likitokea Arusha mjini na kupata ajali hiyo katika wilaya ya Karatu.
Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Therezia Mahingo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Chanzo halisi cha ajali hiyo bado hakijafahamika hadi sasa. Tutaendeleea kuwajuza kuhusu tukio hili.
UPDATES:
Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amethibisha kuwa wanafunzi 31 na walimu wao wamefariki katika ajali iliyotokea wilayani Karatu katika eneo ulipo mto Mlera.
Kamanda Mkumbo amesema kuwa wanafunzi waliofariki ni wa shule ya Luck Vicent ya jijini Arusha na kwamba yupo njiani kuelekea eneo la tukio na atatoa taarifa zaidi akiwasili.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post