USHAURI WA DIAMOND KWA WASANII KUHUSU MBINU ZA KUFANIKIWA KIMATAIFA

Mwanamuziki Diamond Platnumz ambaye mwisho wa wiki alikuwa nchini Zambia katika tamasha la muziki, ametoa ushauri kwa wananumuziki wenzake wa Tanzania juu ya namna ya kutoa nyimbo zao.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond Platnumz amesema kuwa kuna wakati alitoa nyimbo lakini zilipingwa sana sa watu hapa nchini, lakini sababu yeye aliyafahamu malengo yake, alikaa kimya na kwamba nyimbo hizo leo ndio zinampa ‘show’ kubwa za muziki za kimataifa.
“…usiogope kufanya Muziki tofautitofauti ili kuongeza Mashabiki ila ukiogopa kufanya muziki wa mahadhi flani kisa wabongo wataongea na kuamua tu kutoa kina “UKIMUONA” Basi hatutafanikiwa kuteka Masoko na chi zingine..” Aliandika Diamond akiwasihi wanamuziki wenzake kutokuogopa kufanya muziki wa mahadhi mengine tofauti na yaliyozoeleka na Watanzania kwa kuogopa kuwa watakosolewa.
Ujumbe wote unasomeka hivi; Leo ningependa nitoe ujumbe huu kwa wasanii wenzangu pendwa… Siku hizi mjini kila mtu anajifanya yeye soko la Muziki analijua sana na bingwa wa kuelekeza na kukosoa nyimbo za watu….pasipo kujua kuwa kila nyimbo ina soko lake na kila mwanamziki anapotoa nyimbo anakuwa na malengo ama plan ambayo kaidhamilia…leo ntakupostia baadhi ya nyimbo ambazo wakati nazitoa zilidharauliwa, zilipingwa sana na wanaojifanya wajuaji wa Muziki… pasipo kujua kuwa dhamira ama nini yalikuwa malengo yangu….kwakuwa nilikuwa na imani na kufahamu nikifanyacho basi nikawa nawaekea tu neno #MALENGO na leo hii nyimbo hizo ndio sababu kubwa ya mimi kuwa na Show za nchi ambazo kiukweli sijawai tegemea fika na kufanya show za Uwanjani….. sababu yangu kubwa leo ni kuwasihi wasanii wenzangu kuwa mnapokuwa na kitu ambacho mnamalengo ama target nacho msiogope kukisimamia…lakini pia kuwajuza kuwa kila kanda ina maadhi ya muziki wake ambao unaupenda, hivyo ukitaka kufanikiwa kushika kanda zote usiogope kufanya Muziki tofautitofauti ili kuongeza Mashabiki ila ukiogopa kufanya muziki wa mahadhi flani kisa wabongo wataongea na kuamua tu kutoa kina “UKIMUONA” Basi hatutafanikiwa kuteka Masoko na chi zingine… #SimbaInZambia

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post