VIDEO: KAULI YA WAZIRI MWAKYEMBE KUHUSU WASANII WANAOIMBA NYIMBO ZA SIASA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Mwakyembe amewasihi wa Tanzania kuacha kutumiwa na viongozi mbalimbali kwa kuimba nyimbo za masuala ya kisiasa na badala yake wafanye kazi ambazo zitawasaidia kupata mafanikio.
Waziri Mwakyembe aliyasema hayo bungeni wakati akijibu hoja mbalimbali zilizotolewa na wabunge wakati wa kujadili hotuba ya bajeti ya wizara yake.
Tembea dunia kote huko, nimekwenda Nigeria na kuona wasanii wakubwa kama Tiwa Savage, Don Jazz, Akon, P Square wale hawaimbi kuhusu viongozi wao wa kisiasa. Hivyo niwasihi wasanii wangu, muache kuimba kuhusu siasa sababu hii ni ‘entertainment industry’ (sekta ya burudani) na sio ya masuala ya kisiasa, alisema Waziri Mwakyembe.
Aidha, waziri alisema kama kuna msanii yeyote anayetaka kuwa mwanasiasa aache muziki akagombee udiwani kwani wasanii waliotaka kuchanganya siasa na muziki walipotea kabisa.
Lakini kwa upande mwingine kauli hiyo imepokelewa kwa mtazamo tofauti na watu mbalimbali kwenye mitandao huku baadhi wakisema kuwa chama chake (CCM) ndicho huwatumia wasanii wakati wa kampeni za uchaguzi na kwamba hata mpaka sasa hivi bado kinawatumia, kama wanavyofanya kwa Mrisho Mpoti.
Baadhi ya watu wengine walikosoa kauli hiyo ya Waziri Mwakyembe wakisema kuwa , kazi ya muziki ni kuburudisha, kuelimisha na kukosoa hivyo unaweza kutumika sehemu yeyote haijalishi kama ni afya, siasa au uchumi na pia si kweli kwamba duniani kote hakuna wasanii waliofanikiwa wanaoimba kuhusu siasa.
Hapa chini ni maoni ya baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii kuhusu kauli hiyo ya waziri.
Duniani?
Eminem
2 Pac
Jay Z
Nas Escobar
Mos Def
Public Enemy
Dead Prez
Geto Boys
Brother Ali
n.k https://twitter.com/swahilitimes/status/862202159257067520 
Kauli ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Mwakyembe kuhusu wasanii wanaojiingiza katika siasa. pic.twitter.com/BbLSNlPWcP
@swahilitimes Kwa hotuba hii nimeelewa kwa nini roma alitekwa kweli viongozi hawapendi kukoselewa kama hospitl hakuna dawa tusiimbie serikali?
Poor Mwakyembe. Dhima ya muziki sio kuburudisha tu bali pia kuelimisha, kuhamasisha,kukosoa, nk (kutaja machache). Hakusoma fasihi simulizi? https://twitter.com/swahilitimes/status/862202159257067520 
Anko jamani
Naomba nikujibu
1. Majina makubwa na siasa: Angelique Kidjo, Youssou Ndour, Bob Marley, Burning Spear, Tracey Chapman, Beyonce https://twitter.com/swahilitimes/status/862202159257067520 
2. Kuhusu eti successful - tokea lini mafanikio ya msanii yakapimwa kwa pesa na kumiliki ndege? Nadhani kila mtu ana definition yake https://twitter.com/swahilitimes/status/862202159257067520 

Wolfgang Amadeus Mozart alikufa maskini lakini hakuna anayeweza sema hakuwa successful. Opera zake zilikuwa zinakosoa mfalme. https://twitter.com/swahilitimes/status/862202159257067520 
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post