VIDEO: MWANAMKE NCHINI UGANDA AVUNJA REKODI YA KUWA NA WATOTO WENGI ZAIDI

Wakati jamii ikihimizwa kuhusu masuala ya uzazi wa mpango ambao utawawezesha kuwa na watoto wachache ili waweze kumudu kuwapatia mahitaji muhimu ikiwamo elimu, malazi, mavazi na chakula, mwanamke mmoja nchini Uganda ameweka rekodi ya kuwa na watoto wengi zaidi.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 39 huenda ndiye mwenye watoto wengi zaidi barani Afrika ambapo amezaa jumla ya watoto 44 kwa mume mmoja, lakini hadi sasa watoto 38 pekee ndio wapo hai.
Akielezea hali hiyo alisema kuwa amekuwa akijifungua mapacha wengi mara kwa mara na hivyo kufanya idadi kubwa ya watoto, lakini kwa upande wake alitamani kuwa na watoto 6 pekee.
Mama huyo ambaye anaonekana bado ana uwezo wa kuzaaa watoto wengine amesema kuwa mara kadhaa amekwenda hospitali ili afunge uzazi lakini wataalamu wa afya wamemwambia kuwa ana mayai mengi na hivyo ni hatari kwa afya yake kufanya hivyo.
Watoto hao kwa siku moja hula 7kg za maharage, 24kg za unga, na 2.5kg za sukari.JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post