VIDEO: POLISI AMFYATULIA RISASI ALIYEKUWA NAIBU WAZIRI WA FEDHA, ADAM MALIMA

Mchana wa leo imeanza kusambaa video kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha Askari wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania akifyatua risasi angani katika kile kinachodaiwa kuwa alikuwa akizozana na aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha katika Serikali ya Awamu ya Nne, Adam Kighoma Ali Malima
Indaiwa mgogoro huo ulikuwa kati ya Majembe Auction Mart waliokuwa wameambatana na Polisi walipojaribu kukamata gari lilokuwa limeegeshwa pembeni ya barabara hali ya kuwa dereva yupo ndani eneo la Masaki Dar es Salaam.
Taarifa hizi hazijathibitishwa na Jeshi la Polisi, lakini watu mbalimbali walioona makanda huu wa video kwenye mitandao ya kijamii wamekosoa kitendo cha Askari Polisi kutumia nguvu iliyopitiliza katika kumkabilia raia ambaye hakuwa akifanya vurugu wala kuwa na silaha.
Hapa chini ni video ya tukio hilo. Itazame kisha tuandikie maoni yako.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post