VIDEO: SPIKA AKIELEZA MAANA YA TUSI ALILOTUKANWA NA HALIMA MDEE

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai jana ameonyesha kuumizwa na kitendo cha Mbunge wa Kawe kwa tiketi ya CHADEMA Mh. Halima Mdee kutumia lugha chafu dhidi yake wakati wa uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki.
Spika Ndugai alieleza kuwa kwa utamaduni wa Waafrika ni vyema hata kama unamchukia mtu utumie lugha ya staha kumueleza kuliko kutumia matusi.
“Kwa neno ambalo alilisema Halima Mdee humu ndani, kamati imeenda kwenye tafsiri ikachukua Kamusi kwa neno lile alilosema ambalo maana yake kwa yule unayemwambia ‘Fala’ ni mtu ambaye akili zake hazifanyi kazi vizuri, ni mtu mpumbavu, ni mtu bwege, ni mtu mjinga, ni mtu bozi, ni gulagula. Ndiyo maana nikasema sisi Waafrika hata kama humpendi namna gani mwenzako huwezi kumfanyia hivyo” alisisitiza Job Ndugai
Hata hivyo, kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge ilimwita Mbunge Halima Mdee na kuzungumza nae ambapo alikiri kuwa amekosea kutumia lugha chafu dhidi ya Spika wa Bunge na kuomba radhi.
Kamati ilipanga kumpa adhabu ya kutokuhudhuriia vikao vyote vya Bunge la Bajeti vilivyosalia lakini wabunge walimuombea msamaha na kamati ikaridhia kumsamehe Halima Mdee.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post