VIDEO : YANGA YARUDI TENA KILELENI VPL

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Young Africans wametoka vifua mbele baada ya kuwachapa mabao 2-0 wapinzani wao Tanzania Prisons katika mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.


Mabao hayo yote mawili yamepatikana katika dakika 45 za kipindi cha pili cha mchezo huo ambapo ilipofika dakika 71 Amisi Tambwe aliweza kuchungulia nyavu za wapinzani wao kwa mara ya kwanza na kuifanya Yanga kuongoza bao 1-0 na ilipofikia dakika 76 za mchezo Obrey Chirwa aliwainua tena mashabiki wa klabu hiyo kwa kufunga bao la pili na kuifanya timu yake kuibuka kidedea mpaka mpira kuisha.
Kwa matokeo hayo timu ya Yanga imeweza kujiongezea pointi zake 3 na kuifanya kufikia alama 59 sawa sawa na Simba SC.
Katika hatua nyingine Nahodha wa Prisons, Benjamini Asukile amesema pamoja na kufungwa na Yanga bado hawajakata tamaa na Prisons lazima itabaki Ligi Kuu Bara.
“Kuna makosa tulifanya kipindi cha pili na Yanga wakaitumia nafasi hiyo. Lakini tutaendelea kupambana na imani yetu Prisons itabaki ligi kuu”. Alisema Asukile

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post