WABUNGE WA UKAWA WALIODAIWA KUMSHIKA MATITI KATIBU TAWALA WA DAR WAACHIWA HURU

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo imewaachia huru wabunge wa Ukawa na makada wa muungano huo baada ya kuona kuwa hawana kesi ya kujibu.
Wabunge na makada hao walikuwa wakikabiliwa na kesi ya kumjeruhi pamoja na kumdhalilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu,Huruma Shaidi amesema kuwa amewaachia huru watuhumiwa hao baada ya kujiridhisha kuwa hawana kesi ya kujibu.
Hakimu amesema kuwa ushahidi uliotolewa na walal,ikaji umeshindwa kuthibitishwa na hata mlalamikaji anayedai kujeruhiwa hakumbuki ni nani aliyemjeruhi.
Kuhusu madai ya kudhalilishwa kwa kushikwa matiti, ilishindwa kufahamika ni nani alihusika katika kosa hilo na hivyo watuhumiwa wakawa hawana kesi ya kujibu.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post