WABUNGE WANENA HAYA BAADA YA RAIS KUTENGUA UTEUZI WA WAZIRI MUHONGO

Rais Dkt John Pombe leo ametengua uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kwa kile alichosema kuwa ni kushindwa kusimamia wizara hiyo na hivyo kupelekea serikali kupata hasara kufuatia makinika ya madini kusafirishwa kwenda nje ya nchi.
Rais ametoa uamuzi huo baada ya kupokea ripoti kutoka kwa kamati aliyoiunda kuchunguza kiasi cha madini kilichomo kwenye mchanga wa madini unaosafirishwa nje ya nchi.
Baada ya Rais Magufuli kutengua uteuzi huo, watu mbalimbali wakiwamo viongozi na wabunge wamekuwa na maoni mbalimbali juu  ya kutengua uteuzi huo na pia kuhusu ripoti iliyowasilishwa kwake leo. Hapa chini ni baadhi ya maoni kutoka kwenye mitandao ya kijamii.
Utafiti unapingwa Kwa utafiti. KWA SASA Kamati ya Mruma Ndio rejea sahihi kwenye suala la Mchanga na hivyo NAKUBALI mapendekezo yaliyomo https://twitter.com/henrymsuya1/status/867288820244504577 
Kama hawakujua kuwa tunaibiwa, two things: conspiracy (walikuwa sehemu ya deal) ya muda mrefu ambapo walikuwa wakirithishana au 'ignorance'!
Ni ngumu sana kuamini kwamba 'wasomi' wetu hawakuwa wanajua kwamba tunaibiwa. Wabunge tulisema tukaonekana mbumbumbu! 
Sishangai kumsikia Rais wetu akisema 'Wasomi' tumeiangusha nchi. Kwa kila namna tunapaswa kujitazama sana! 

Nimemsikiliz Mheshimiwa Raisi na kuendelea kuielewa Nia yake njema ya kuisaidia Nchi yake. Tuko pamoja na ninakuunga mkono
Thank u Mr President this is a noble Job tunaotoka maeneo ya Madini tunaelewa madhara ya huu uwekezaji.
Haya ni mapambano ya kiuchumi dhidi ya Ubepari , Idara yetu ya Usalama inawajibu mkubwa sana ktk vita hii ya ku Linda Rasilimali.
Rais Magufuli anafanya siasa na hapaswi kuaminiwa na mtu yeyote kuhusu suala hili la madini. Tatizo kubwa katika sekta ya madini ni sheria.
Magufuli will appoint Kalemani to replace Muhongo... Wait and see


JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post