WAFANYABIASHARA WATOA MADUKUDUKU YAO MBELE YA RAIS DKT MAGUFULI

SHARE:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 06 Mei, 2017 amezindua Baraza la Taifa la Biashara (TNBC...

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 06 Mei, 2017 amezindua Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) na kuongoza Mkutano wa 10 wa Baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Baraza hili ni la tatu na mkutano huu ni wa kwanza kuongozwa na Mhe. Rais Magufuli tangu aingie madarakani ambapo tofauti na mikutano mingine, Mhe. Rais Magufuli ameendesha majadiliano ya pamoja ambapo wajumbe wa baraza na wawakilishi wengine kutoka sekta binafsi wamepata fursa ya kutoa maoni, mapendekezo na dukuduku, kisha kupatiwa majibu kutoka kwa Mawaziri, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na Mhe. Rais.
Miongoni mwa yaliyojitokeza ni kuiomba Serikali kuendelea kushirikiana na sekta binafsi katika upangaji na utekelezaji wa mipango, sera na sheria mbalimbali za uwekezaji na biashara, kuendelea kuondoa vikwazo na urasimu ambao unachangia kupunguza ufanisi katika biashara na uwekezaji, kuongeza vivutio vya uwekezaji na kuendelea kushirikisha sekta binafsi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi, utalii na viwanda.
Aidha, wawakilishi wa sekta binafsi wameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa juhudi kubwa inazozifanya kujenga miundombinu muhimu kwa uwekezajina biashara kama vile ujenzi wa reli, barabara, meli na ununuzi wa ndege, kukabiliana na rushwa, kusimamia mpango wa ujenzi wa viwanda, kujenga nidhamu na uwajibikaji wa watumishi wa umma na kujenga uhusiano mzuri na mataifa mbalimbali duniani.
Pamoja na majibu yaliyotolewa na Mawaziri ambao ni wajumbe wa Baraza la Taifa la Biashara, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amewaahidi wawakilishi wa sekta binafsi waliohudhuria mkutano huo kuwa Serikali itahakikisha maoni yao yote yanafanyiwa kazi ili Taifa liweze kunufaika na rasilimali zake na kusonga mbele kimaendeleo.
“Naomba niwahakikishie kuwa hisia zenu tumezipata, maoni yenu tutayazingatia na tutahakikisha tunayafanyia kazi haraka iwezekanavyo ili kwa pamoja tufanye kazi ya kuijenga nchi yetu” amesema Mhe. Majaliwa.
Mhe. Rais Magufuli amewapongeza wajumbe wa Baraza la Taifa la Biashara pamoja na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) inayoongozwa na Mwenyekiti wake Dkt. Reginald Mengi kwa juhudi kubwa zinafanywa kuendeleza biashara na uwekezaji nchini na amewaahidi kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kuwathamini na kushirikiana na wawekezaji na wafanyabiashara kwa manufaa ya Taifa.
Mhe. Rais Magufuli ameelezea kufurahishwa na maoni, mapendekezo na dukuduku alizozipata kutoka kwenye mkutano huo na amewakikishia kuwa Serikali anayoiongoza itafanyia kazi maoni yote yaliyotolewa ikiwemo kuondoa usumbufu unaosababishwa na uwingi wa taasisi zinazomhudumia na kumtoza mfanyabiashara na mwekezaji, kuongeza vivutio, kuboresha mifumo ya ukusanyaji wa kodi mbalimbali na kuishirikisha sekta binafsi katika mipango na utekelezaji wa miradi.
Kuhusu tatizo la ucheleweshaji wa mizigo bandarini Mhe. Rais Magufuli ameagiza kuanzia Jumatatu tarehe 08 Mei, 2017 taasisi zote zinazotoa huduma katika bandari ya Dar es Salaam ziungane na Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kutoa huduma kwa muda wote wa saa 24.
“Kama alivyosema Waziri Mkuu, tunataka kufanyia kazi maoni yenu mara moja, kuanzia Jumatatu nataka taasisi zote za pale bandarini zitoe huduma saa 24, haiwezekani bandarini kwetu mizigo ichukue siku 13 kuitoa bandarini wakati bandari za wenzetu majirani inatoka baada ya siku 3, tutashindana vipi?” amehoji Mhe. Rais Magufuli.
Hata hivyo Mhe. Dkt. Magufuli amewataka wafanyabiashara na wawekezaji wajirekebisha kwa kasoro ambazo baadhi yao wanazo ikiwemo ukwepaji wa kodi, kupandisha viwango vya bei kwa huduma wanazotoa Serikalini, kujihusisha na rushwa, kutaka faida kubwa isiyostahili bila kuwajali wananchi na kutochangamkia fursa za uwekezaji za ndani na nje ya nchi licha ya juhudi zake za kuwaleta viongozi na wafanyabiashara kutoka nchi mbalimbali.
“Nataka mjiulize amekuja Waziri Mkuu wa India, amekuja Rais wa Vietnam, amekuja Rais wa Uturuki, amekuja Rais wa Kongo (DRC), amekuja Rais wa Zambia, amekuja Rais wa Uganda, amekujaMfalme wa Morocco na wengine wengi, tumenufaikaje? Mbona wao wanakuja kuwekeza hapa nyie kwa nini hamuendi kwao?” amehoji Mhe. Rais Magufuli.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
06 Mei, 2017

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: WAFANYABIASHARA WATOA MADUKUDUKU YAO MBELE YA RAIS DKT MAGUFULI
WAFANYABIASHARA WATOA MADUKUDUKU YAO MBELE YA RAIS DKT MAGUFULI
https://3.bp.blogspot.com/-t2IH7CkMjQw/WQ4vkum_UjI/AAAAAAAAavY/r9bYjY9VIngKyWg0UGGml9jLv1yFyYBYQCLcB/s1600/C_JQY_VXgAIwixJ.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-t2IH7CkMjQw/WQ4vkum_UjI/AAAAAAAAavY/r9bYjY9VIngKyWg0UGGml9jLv1yFyYBYQCLcB/s72-c/C_JQY_VXgAIwixJ.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/05/wafanyabiashara-watoa-madukuduku-yao.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/05/wafanyabiashara-watoa-madukuduku-yao.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy