WAGOMBEA 6 WALIOTEULIWA NA CHADEMA KUGOMBEA UBUNGE WA AFRIKA MASHARIKI

Baada ya wagombea wake wawili kukataliwa katika awamu ya kwanza ya uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa orodha mpya ya wananchama wake 6 watakaogombea nafasi hiyo.
Hatua hii ya CHADEMA kutangaza wagombea wengine imekuja baada ya wagombea wawili wa awali kutokukidhi vigezo vya msharti ya kupigiwa kura ambao uteuzi haukuzingatia jinsia na wala hakukuwa na ushindani sababu wagombea waliopelekwa ni wawili na nafasi zilikuwa mbili.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana usiku na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa CHADEMA, Tumaini Makene, amewataja wagombea hao kuwa ni Profesa Abdalla Safari, Salum Mwalim, Ezekiel Wenje, Josephine Lemoyan, Lawrence Masha pamoja na Pamela Massay.
“Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyokutana Zanzibar katika kikao chake cha siku moja, Mei 2 mwaka huu, imeadhimia kuwateua wakilishi wa CHADEMA kugombea Ubunge wa Afrika Mashariki (EALA)”. Alisema Makene kwenye taarifa yake aliyoitoa
Uchaguzi wa wabunge hao utafanyika Mei 10 mwaka huu ili kuweza kuwapata wawili watakaoungana na wenzao 7 kuiwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post