WAKAZI WA DODOMA WAJAWA HOFU BAADA YA NDEGE KUPITISHWA KWENYE BARABARA YA MAGARI

Wakazi wa Dodoma jana waliingiwa na hofu baada ya kuona ndege ndogo iliyokuwa ikivutwa na trekta kwenye barabara ya magari, huku wengine wakidhani ilipata hitilafu ikiwa angani hivyo kutua katikati ya barabara.
Muda mfupi tu baada ya ndege hiyo kuonekana barabarani zilianza kusambaa picha zikiwa na maelezo ya kwamba ilitua barabara, huku wengine wakisema ni ndege ya Tanzania imetua huko Mombasa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, ndege hiyo haikutua barabarani kama ilivyodaiwa bali ilikuwa ikipelekwa kwa mmiliki wake ambaye anamiliki African Dream Hotel baada ya kuinunua ambapo alikuwa akiitoa uwanjani kuipeleka Area D.
Baada ya baadhi ya watu kuhoji kama ndege hiyo ikihitaji kuruka italazimika tena kuburuzwa hadi uwanja wa ndege, Waziri wa Ujenzi Prof. Mbarawa alisema, ndege hiyo ni mbovu na imetolewa uwanjani baada ya kuuzwa, na huko inakoenda haitoruka tena itatumika kama kivutio tu.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post