WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUKUTANA KESHO DAR ES SALAAM

Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kesho wanatarajia kukutana na kufanya mazungumzo ya pamoja ya mkutano wa 18 utakaofanyika hapa nchini, Ikulu ya Jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo unatarajiwa kupokea ripoti ya usuluhishi ya kamati iliyoongozwa na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa kuhusu mgogoro wa Burundi.
Mambo mengine yanayotarajiwa kuzungumziwa katika mkutano huo ni pamoja na taarifa na maelekezo mbalimbali yaliyotolewa katika mkutano wa 17 wa wakuu wa nchi za Jumuiya hiyo.
Taarifa hiyo ni pamoja na namna ya kuwezesha uundaji wa magari katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kupunguza uagizaji wa magari yaliyotumika kutoka nje ya Jumuiya, mapitio kuhusu sekta ya nguo pamoja na ngozi.
Masuala mengine ni pamoja na kuzuia ama kuondoa kabisa uagizaji wa nguo na viatu vya mtumba kutoka mataifa ya nje.
Wakuu hao wa Nchi pia wanatarajia kujadili namna endelevu ya uchangiaji wa bajeti ya Jumuiya hiyo kwa nchi wananchama.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post