WANAFUNZI WAKIKE 82 WALIOTEKWA WAACHIWA NA KUNDI LA BOKO HARAM

Wanamgambo wa kundi la Kiislam la Boko Haram wamewaachia wanafunzi wa kike 82 kati ya 276 waliotekwa kaskazini mashariki mwa Nigeria miaka mitatu iliyopita.

Ofisi ya rais imesema wanafunzi hao wameachiwa katika makubaliano ya kubadilishana na watuhumiwa wa kundi la Boko Haram baada ya mazungumzo.

Wasichana hao watapokelewa na rais wa Nigeria Muhammadu Buhari katika Jiji la Abuja siku ya leo, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa.

Kabla ya kuachiwa kwa wanafunzi hao wa kike, wanafunzi 192 walikuwa bado hawajapatikana tangu walipotekwa.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post