WANANCHI WAMTAKA JPM KUENDELEA KUTUMBUA WENYE VYETI FEKI

Katika kuhakikisha kuwa hatua zinazochukuliwa na Rais Dkt. Magufuli za kutumbua watumishi wenye vyeti vya kufoji, Wananchi wameonekana kuunga mkono hatua hiyo ili kuweza kupunguza gharama kubwa ambazo zimekuwa zikitumiwa na Serikali kuwalipa watumishi hao ambao hawastahili.
Zote Kali imefanya mahojiano na baadhi ya wananchi ambao wamesema kuwa hatua hiyo mi nzuri na wanamuunga mkono Rais Dkt. Magufuli kwani kufanya hivyo inasaidia taifa kuepukana na matumizi makubwa ya fedha yasiyokuwa na msingi wowote.
“Tuna muunga mkono Rais Dkt. Magufuli kwa kazi anayoifanya kwani hata kwenye kampeni zake alisema anataka kuongoza nchi iliyonyooka , hivyo haiwezekani Tanzania kuwa ni nchi ya Viwanda halafu wataalamu wake wamefoji vyeti,”amesema Hassan.
Aidha, Rais Dkt. John Magufuli  alikabidhiwa orodha ya wafanyakazi ambao wanatumia vyeti vya  kughushi na kuagiza mara moja wajiondoe kazini kabla hajaanza kuwashughulikia ifikapo tarehe 15, Mei mwaka huu.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post