WATANZANIA WENGI HAWANUFAIKI NA MADINI SABABU YA VIONGOZI WAO

Mkuu wa mkoa wa Manyara Dk Joel Bendera akifatilia jambo wakati alipokuwa anazindua rasmi maonyesho ya sita ya vito na madini yanayofanyika katika hotel ya Mounti Meru iliyopo jijini Arusha(habari picha na Woinde Shizza,Arusha)
 Meya wa jiji la Arusha naye aliuzuria katika uzinduzi wa maonyesho haya ya vito na madini
Na Woinde shizza,Arusha
Wananchi wengi wanaoishi karibu na migodi mbalimbali inayochimba madini ya aina mbalimbali wamekuwa hawanufaiki kupitia madini hayo kutokana na viongozi wao wa maeneo husika kutokuwa na uhusiano mzuri na wamiliki wa migodi hiyo.
Hayo yamebainishwa na mbunge wa jimbo la Simanjiro Jemsi ole milya wakati akiongea katika uzinduzi wa maonyesho vito na madini yaliofunguliwa leo jijini hapa
Alisema kuwa japo kuwa madini mengi yenye dhamani yanachibwa hapa nchini lakini ukifuatilia maisha ya wananchi wa maeneo ambayo madini hayo yanatoka hayafanani kabisa nao kwani asilimia kubwa ya wananchi hao ni maskini sana na wengine awajiwezi
“asilimia kubwa ya wananchi ambao madini hayo yanachibwa ukifatilia maisha yao hayafai kwani ni duni hawana maendeleo yoyote ,kwa ufupi awanufaiki na madini ambayo yanatoka katika maeneo yao hivyo ni wajibu waserikali kuangalia upya swala hili na kuanza kufatilia kwani ni kitu cha kusikitisha unakuta mwananchi mfano wa Mererani madini yanachibwa kwao lakini ukiangalia maisha anaoyoishi uwezi sema anakaa sehemu Tanzanite inatokea kwa jinsi anashida”alisema Milya
Naye kaimu naibu katibu mkuu wa wizara ya Nishati na madini Jemsi Mdoe alisema kuwa sera ipo na sheria ipo ya kuakikisha wananchi ambaowanazunguka maeneo ya migodi wanasaidiwa na migodi hiyo lakini ukifuatilia kwa kiasi kikubwa wale wananchi ambao hawanufaiki ni wale ambao unakuta viongozi wao wa mtaa au kijiji awanaushirikiano mzuri na viongozi au wawekezaji waliowekeza katika maeneo yao ,hivyo ni wajibu wawanchi pamoja na viongozi kushirikiana kwa pamoja na kuungana ili kuweza kusaidia
Akizungumzia maonyesho haya ya madini ya vito (Arusha Gem Fair )alisema kuwa haya ni maonyesho ya sita kufanyika na yanafanyika kwa muda wa siku tatu lengo ikiwa kutimiza dira iliopo katika sera ya madini ya mwaka 2009 inayosisitiza kuwa Tanzania iwe kitovu cha madini .
Alisema kuwa sekta ndogo ya vito inachangia katika uchumi wa maendeleo ya jamii hivyo maonyesho haya ni fursa kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa hapa nchini kuweza kupata fursa ya kujitangaza zaidi
“unajua wageni wengi kutoka nchi mbalimbali wanauthuria katika maonyesho haya wengine wanakuja kununua madini wengine wameleta madini yao ili yauzwe kwaiyo hii ni fursa ya pekee ya wachimbaji wetu wa ndani kujitangaza na kupanua soko la zaidi kikubwa zaidi waangalie ni namna gani watayafanya madini yao yawe na dhamani zaidi”alisema Jemsi.
Baadhi ya madini yaliyoletwa katika maonyesho

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post