WATU 21 WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA MGODI

Waokoaji nchini Iran wameopoa miili ya watu 21 baada ya kutokea mlipuko mkubwa katika mgodi mmoja wa makaa ya mawe, huku zaidi ya wengine 69 wakijeruhiwa.

Mlipuko huo unadhaniwa kusababishwa na kuvuja kwa gesi katika mgodi wa Zemestan-Yurt Kaskazini mwa jimbo la Golestan. Baadhi ya miili hiyo ni ya watu waliokwenda katika mgodi huo kuwasaidia waliojeruhiwa.


Zaidi ya wachimbaji wengine 32 wamekwama ardhini. Juhudi za uokoaji zinaendelea huku zikikwamishwa na njia nyembamba ya kuingia sambamba na uwepo wa kiwango kikubwa cha gesi ndani ya mgodi huo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post