WAWILI WAFARIKI NDANI YA MGODI IRINGA

Wachimbaji wawili wa madini katika Kijiji cha Masuluti mkoani Iringa, wamefariki dunia ndani ya mgodi walimokuwa wakichimba.
Wachimbaji hao waliotajwa kwa majina kuwa ni James Mlawa (22) mkazi wa Kijiji cha Magulilwa, Iringa pamoja na Haus Kaijage (32) mkazi wa Kigoma wamefariki baaada ya kile kilichodaiwa kuwa ni kukosa hewa ndani ya mgodi huo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Julius Mjengi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa tayari miili ya marehemu imeshatolewa katika mgodi huo.
Kamanda Mjegi amesema chanzo cha watu hao kupoteza maisha ni baada ya kukosa hewa kulikosababishwa na jenereta la kuvutia maji waliloingia nalo ndani ya mgodi na kuliwasha kwa lengo la kutoa maji nje.
Mtendaji wa Kijiji cha Masuluti, Venjaslaus Kiunosile alieleza kuwa tukio hilo limetokea leo Mei 19 majira ya saa tano asubuhi.
Naye Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Mgama, Baraka Mwifune ameeleza kwamba uchunguzi wa awali uliofanyika umebaini kuwa marehemu hao walifariki kwa kukosa hewa.
Samwel Msigwa ambaye ndiye mmiliki wa mgodi huo alisema kwamba akiwa njiani kuelekea eneo la mgodi huo kwa ajili ya kusaidia kutengeneza mashine ya kuingiza hewa ndani ya mgodi wake ndipo alipopata taarifa kuwa wachimbaji wawili kati ya sita waliokuwa wameingia humo wamefariki kwa kukosa hewa.
Hata hivyo jeshi la Polisi bado linamshikilia Msigwa kwa ajili ya mahojiano zaidi.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post