WAZIRI MWIGULU NCHEMBA ASEMA SERIKALI HAINA SHERIA YA KUZUIA SHISHA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema kuwa serikali bado haina sheria ya kudhibiti, uingizaji, usambazaji na matumizi ya kilevi aina ya shisha.
Waziri Nchemba ameyasema hayo leo bungeni ambapo ameeleza kwamba licha ya kuwa sheria hiyo haipo, lakini kuwa agizo la Waziri Mkuu la kupiga marufuku biashara hiyo na kutaka agizo hilo lifuatwe na kila mtu.
Mwigulu Nchemba amesema hayo alipokuwa akijibu swali kuhusu matumizi ya kilevi hicho cha shisha ambacho bado katika baadhi ya maeneo kimeendelea kutumika na kuleta athari kwa watumiaji licha ya kuwa serikali imepiga marufuku.
“Ni kweli serikali baada ya kuona matumizi ya kilevi cha Shisha yanaleta athari kwa binadamu, serikali imeanza kuweka sheria za kuthibiti matumizi ya shisha, usambazaji wa shisha na uagizaji wa kilevi hicho, lakini wakati tunasubiri sheria hizo tunatambua kuwa lipo agizo la Waziri Mkuu la kupiga marufuku matumizi ya kilevi cha shisha ambalo utekelezaji wake ulianza mikoani kama Dar es Salaam, Mbeya, Iringa na mikoa mingine imeendelea kuitikia. Kwa hiyo maelekezo ya Mh. Waziri Mkuu yanafanyiwa kazi bila kupunguza hata nukta” alisema Mwigulu Nchemba
Mbali na hilo Waziri Mwigulu alisema anatambua wapo watu walipewa leseni kwa ajili ya kufanya biashara hiyo ya shisha lakini kwa kuwa serikali inajali masuala ya afya ya Watanzania ndiyo maana wanatakakuja na sheria ili kuthibiti kilevi hicho ambacho kina athari kwa watumiaji.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

SHARE THIS

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post