WAZIRI WA MASUALA YA JAMII NA KAZI”ABAS ABDULAH” AUAWA KWA KUPIGWA RISASI KARIBIA NA IKULU YA RAIS

Waziri mwenye umri mdogo zaidi nchini ameuawa kwa kupigwa risasi mjini Mogadishu. Abas Abdullahi Sheikh Siraji aliyekuwa na miaka 31 ameuawa karibia na ikulu ya Rais. Abas Abdullahi Sheikh Siraji hakuwa waziri wa kawaida nchini Somalia. Alipata umaarufu mkubwa baada ya kushinda kiti cha ubunge na kuiwakilisha Jubbaland.
Alikuwa waziri wa masuala ya jamii na kazi huku watu wengi wakimtaja kama mtu machachari sana miongoni mwa mawaziri.
Saa chache kabla ya kuuawa kwake alizindua mradi wa ujenzi wa jengo kwa ajili ya watumishi wa umma.
Waziri wa habari wa Somalia amesema kuwa washukiwa wa mauaji hayo wamekamatwa.
Huyo ni waziri wa Somalia

CHANZO:BBC
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post