WEST HAM YAITIBULIA TOTTENHAM MAHESABU YA KUFUKUZIA UBINGWA

Mbio za Tottenham kuwafukuzia vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza timu ya Chelsea zimepata pigo kufuatia kufungwa goli na Manuel Lanzini lililoipatia West Ham ushindi.

Tottenham wangeweza kupunguza pengo na vinara hao na kubakia tofauti ya pointi moja tu iwapo wangeshinda katika dimba la London Stadium jana, lakini wakajikuta wakilala.

Katika mchezo huo kipa wa wagonga nyundo wa London, Adrian aliokoa kwa ubora wa juu mipira iliyopigwa na Harry Kane na Eric Dier kabla ya Lanzini kufunga.

Kwa matokeo hayo West Ham wameisaidia Chelsea kuukaribia zaidi ubingwa na sasa inahitaji kushinda michezo yake mwili tu ili kutawazwa kuwa mabingwa.
      Manuel Lanzini akiwa ameachia shuti na kufunga goli pekee katika mchezo huo
           Wachezaji wa Tottenham wakiwa wametingwa na mawazo baada ya kufungwa 
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

SHARE THIS

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post