WHATSAPP KUTUMIKA KATIKA UPASUAJI

Madaktari wa Hospitali ya Aga Khan na Prince Aly Khan nchini India, wanatarajia kuboresha huduma za upasuaji wa mifupa na majeraha kwa kutumia mtandao wa What’sApp.
Teknolojia hiyo mpya inatarajiwa kuanza kutumika nchini baada ya madaktari bingwa kutoka India kuwasili. Madaktari hao kutoka Hospitali ya Prince Aly Khan waliwasili nchini jana kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wenzao wa Hospitali ya Aga Khan kutumia teknolojia hiyo ya kisasa kufanya upasuaji.
Daktari bingwa wa upasuaji mifupa na majeraha wa Hospitali ya Aga Khan, Harry Matoyo amesema madaktari hao walioanza upasuaji wataondoka Jumatatu na kwamba, wanatarajia wataalamu wa hospitali hiyo watakuwa wamenufaika na uzoefu watakaopata.
“Tumetengeneza group (kundi) la What’sApp ambalo litatumiwa na madaktari bingwa wa upasuaji mifupa kati ya nchi hizi mbili, kwa ajili ya kusaidiana iwapo tutakwama wakati wa upasuaji. Tunaweza kupiga picha na kuuliza kitu kinachotakiwa kufanyika,” alisema Dk Matoyo.
Pia, alisema jambo hilo litasaidia kupunguza idadi ya wagonjwa wanaokwenda kutibiwa nchini India, ambao hutumia fedha nyingi.
“Kuna utaalamu mpya wa kutumia kompyuta kufanya upasuaji kama goti ambalo limeharibika vibaya, kuna uwezekano mkubwa wa kulitengeneza upya kwa kutumia teknolojia hiyo. Awali hilo lilionekana ni jambo lisilowezekana” alisema DK Matoyo.
Daktari bingwa wa upasuaji wa mifupa (ubadilishaji wa nyonga bandia na magoti), julius Dinda alisema ni zaidi ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa huduma ya upasuaji wa mifupa, lakini matatizo yamekuwa yakiongezeka kutokana na kutumia mbinu za kizamani.
“Wagonjwa wamekuwa wakiongezeka kutokana na matangazo mbalimbali na elimu inayotolewa kwa wananchi, hivyo kufanya hospitali zinazotoa huduma hizo kuelemewa na idadi kubwa ya wagonjwa” alisema Dk. Dinda.
Dk Dinda alisema madaktari hao wataongeza uwezo hasa kwa kupata mbinu mpya kutoka kwa wataalamu bingwa kutoka India, hali itakayosaidia kupunguza idadi ya wagonjwa waliokuwa wakikaa muda mrefu wakisubiria kupatiwa huduma.
Ofisi ya mtendaji Mkuu kutoka hospitali ya Prince, Ally Khan iliyopo jijini Mumbai, India, Sanjay Oak alisema licha ya kubadilishana uzoefu, itasaidia kuondoa tatizo la wagonjwa kusubiri muda mrefu.
“Jana nilifanya upasuaji wa wagonjwa wawili kwa kutumia njia ya kisasa, leo Dk Fahad Shaikh atafanya upasuaji kwa watoto wawili,” alisema Oak.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post