ZIARA YA KATIBU WA NEC ITIKADI NA UENEZI MH HUMPHREY POLEPOLE WILAYA YA LONGIDO

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Mh. Humphrey Polepole  amefanya ziara ya kukiimarisha chama cha mapinduzi CCM  katika wilaya ya Longido na kuzungumza na wanaCCM wakiwamo wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya 
Mheshimiwa Polepole alifuatana na Viongozi wa Mkoa Akiwamo Mwenyekiti wa CCM  (M) Arusha Mh. Lekule Laizer, Katibu wa CCM  (M) Arusha Ndg. Elias Mpanda, Katibu wa Uenezi Mkoa Ndg.Shaaban Mdoe, Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Arusha Fatuma ,  Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha Ndg.Robert PJN Kaseko na Makada wengine wa CCM Akiwamo Veraikunda Urio.
1. Serikali imedhamiria haswaa kuimarisha sekta ya usafiri wa anga ( ATCL ) kwa kuagiza ndege zingine ili kufikia ndege saba ikiwamo ndege kubwa ya kubeba abiria wasiopungua300, ndege tatu zenye uwezo wa kubeba abiria 102 kila moja ambazo zitasaidia kukuza  sekta ya utalii nchini ili kuliingizia taifa fedha za kigeni.

2. Serikali italeta kwa wananchi tani 500 za chakula kwa bei nafuu ili kuwasaidia wananchi wasio na uwezo  wa kumudu bei za chakula sokoni. kwa mujibu wa mheshimiwa Polepole Chakula hicho kitaanza kuingia juma lijalo.

3. Tutapambana kufa na kupona ili kurejesha ccm jimbo la longido na kata zake zote zilizobebwa na wapinzani.

4. Mradi mkubwa wa maji kusainiwa tarehe 06/05/2017 ili kuwaletea wanachi wa longido huduma ya maji na kuwaondolea kabisa shida ya maji na tatizo kuwa historia. Mradi huo utatoa maji kutoka West Kilimanjaro wilaya ya Siha.

5. Kiwanda kikubwa haswaa cha kutengeneza viatu kujengwa moshi Kilimanjaro na kwamba wamasai sasa wajiandae kupata soko kubwa la ngozi ya ng’ombe zitakazohitaji katika kiwanda hicho.

6. Chama cha mapinduzi kimepanga kujenga chuo kikubwa cha uongozi kwa ajili ya wanaccm na kwamba yeyote mwenye ndoto ya kuwa kiongozi ni lazima apitie chuo hicho.

7. Mheshimiwa Polepole ameguswa na Changamoto mbalimbali zinazoikabili CCM Longido ikiwamo Kukosa Ofisi ya Chama yenye kukidhi mahitaji ya sasa na hivyo Kuchangia Tsh. 500,000/= kwa ajili ya Shughuli za Ujenzi. Tuungane pamoja kukijenga Chama.

8.Mheshimiwa Polepole ametoa rai kwa Wanaccm kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa ndani wa Chama cha mapinduzi unaendeleaje nchini kote. Ametutaka tuchague viongozi wenye mapenzi mema na nchi yetu na Taifa kwa Ujumla, wenye vigezo stahiki & Waadirifu. Tusiwape nafasi Watoa rushwa ambao hutumia pesa zao kusaka uongozi. Hili halikubaliki hata kidogo.
 
 
 
 
 
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

SHARE THIS

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post