ZIFAHAMU TIMU 3 ZILIZOSHUKA DARAJA NA 3 ZILIZOPANDA LIGI KUU TANZANIA

Ligi Kuu ya Tanzania Bara imefikia ukingoni Jana baada ya timu kucheza michezo yao ya 30 ili kuhitimisha mzunguko wa mwisho ambapo Klabu ya Yanga ndio walioibuka mabingwa kwa msimu wa tatu mfululizo.
Klabu ya Yanga imetwaa kombe hilo baada ya kujikusanyia alama 68 katika michezo 30 iliyocheza ambapo licha ya kulingana alama na Simba, lakini wamewazidi katika magoli ya kufunga na kufungwa. Kwa ubingwa wa leo, Yanga inajikusanyia kabatini kombe la 27.
Mbali na Yanga kusherehekea ubingwa, timu nyingine nazo zimesherehekea kubaki ligi kuu baada ya kuwa kwenye nafasi mbaya, ambapo miongoni mwa timu hizo ni Mbao iliyojikusanyia alama 33 katika michezo 30.
Timu zilizoshuka daraja ni African Lyon yenye alama 32, Toto African ya Mwanza yenye alama 30, na JKT Ruvu yenye alama 23 baada ya zote kucheza michezo 30.
Kwa upande mwingine, timu zilizopanda daraja kuingia ligi kuu katika msimu wa 2017/2018 ni Singida United ya mkoani Singida, Lipuli FC ya mkoani Iringa na Mji Njombe.
Licha ya Yanga kutwaa ubingwa wa VPL hawakuonekana kuwa na furaha sana, kwanza kwa sababu wamepoteza mchezo wao wa mwisho dhidi ya Mbao FC baada ya kukubali kipigo cha goli 1-0, lakini pili ni rufaa ya Simba ambayo inadaiwa kuwa imewasilishwa FIFA. Kama FIFA watatoa maamuzi tofauti na yaliyotolewa na TFF, ni dhahiri Simba watapewa alama 3 na kufikisha jumla ya alama 71 hivyo kuwa mabingwa.
Kama Yanga wangeshinda mchezo wa leo, wangejihakikishia ubingwa usio na mashaka kwani hata FIFA wakiipa Simba alama 3, bado Yanga wangewazidi kwa wingi wa magoli.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post