ZITTO KABWE AIJUTIA KAULI ALIYOITOA BAADA YA MATOKEO YA UCHAGUZI WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI

Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa ana wasiwasi na uwezo wa wabunge watakaoiwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki, ikilinganishwa na wabunge wa nchi nyingine.
Zitto Kabwe ambaye amesema kuwa jana baada ya matokeo alikerwa kiasi cha kujutia uraia wake, amesema kuwa nchi nyingi zimepeleka watu wenye uwezo mkubwa sababu Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa sasa ipo katika hatua ya kutumia safaru moja, hivyo ni lazima uwe na watu wenye uwezo. Lakini alionyesha kusikitishwa na wabunge waliochaguliwa kutoka Tanzania.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Zitto amendika;
Jana usiku nilikuwa nimekwazika kufuatia matokeo ya uchaguzi wa wawakilishi wa Tanzania kwenye Bunge la Afrika Mashariki ( EALA ). Kufuatia hasira hiyo nikaandika kuwa wakati mwengine unajiuliza Kama unastahili kuwa kwenye nchi ambayo umo Kama raia.
Haikuwa sahihi Kabisa Kwa Kiongozi wa ngazi yangu kujutia uraia wangu kwa sababu tu ya kundi la watu wachache kuamua kuchagua wawakilishi wetu kwenye taasisi za kimataifa bila kujali uwezo, uzoefu na weledi wa wawakilishi husika.
Ninajua hatua ya Sasa ya Mtangamano wa Afrika Mashariki Ni hatua muhimu mno kwani Ni hatua ya kuelekea Umoja wa Fedha ( Monetary Union). Ndio maana Mataifa mengine yamepeleka raia wao mahiri Kabisa. Rwanda wamepeleka Waziri Mkuu mstaafu na Mawaziri 2. Burundi imepeleka Waziri wake Wa Afrika Mashariki. Uganda imepeleka Mawaziri Wastaafu. Kenya imepeleka Wabunge wazoefu na Wafanyabiashara wakubwa. Hata mwanachama mpya Sudani ya Kusini imepeleka Waziri wa zamani, Spika wa Bunge wa zamani na Jenerali wa Jeshi.
Hasira za kuipenda nchi yangu Ndio zilinipelekea kuandika nilivyoandika. Naomba radhi kwa andiko lile na ninalifuta. Hata hivyo, Wabunge wote wa vyama vyote wajue kuwa wameionea Nchi yetu. Wameweka maslahi ya vyama vyao na mahusiano yao mbele ya maslahi ya nchi yetu. Tanzania imepeleka ‘amateurs’ huko EALA. Huu ndio ukweli mchungu na lazima usemwe. Itabidi kuwa na program maalumu ya kuwafundisha wawakilishi wetu hawa. Kina Adam Kimbisa lazima wachukue jukumu hili bila kujali usumbufu wake.
Anyways! My country, Right or Wrong.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post