ACT WAZALENDO : ZITTO AWEZI KUZIBWA MDOMO

Chama Cha Act-Wazalendo kimesema kuwa wanasiasa wanaolitumia jina la Chama hicho na Kiongozi wa Chama, Zitto Kabwe kwa ajenda zao na propaganda mbaya wamefeli.
Hayo yamelezwa na Katibu wa Vijana wa Chama hicho Mkoa wa Kagera, Khalfani Fadhili na kudai kuwa Chama hicho  hakitarudi nyuma na kwamba hawatayumbishwa na propaganda za wanasiasa wenye nia ovu na chama hicho.
Propaganda hizo ni pamoja na kukihusiha chama hicho na Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja kumtaja na kiongozi kuwa atapewa nafasi kubwa kwenye Serikali ili kukiua chama hicho.
Amesema kuwa baadhi ya kauli za wanasiasa kuwa Zitto Kabwe atafungwa mdomo kwa kupewa nafasi ndani ya Serikali  kuwa sio za kweli na hazina afya kwenye siasa nchini.
“Zitto sio mmiliki wa  ACT wazalendo bali  ni mwanachama wa  ACT na ni  mbunge mwenye dhamana ya chama, pia ni  kiongozi mkuu katika chama. Hivyo ukikuta mwanasiasa mwenye nia ovu  kwa kauli zao za kuwaaminisha watu kuwa Zitto yuko mbioni kupewa Uwaziri ili Act-Wazalendo ife jua huyo ni mwanasiasa aliyefilisika,” amesma.
Ameongeza kuwa wapo wanaowaaminisha watu kuwa Act-Wazalendo ni sehemu ya CCM ilhali chama cha Act kina sera za kulijenga taifa, ujamaa na uzalendo kwa kushirikiana na watanzania wote bila kujali itikadi zao.
“Sikatai kuwa haiwezekani kuwa akapewa nafasi nyeti katika serikali hii inayoonyesha kuguswa na viongozi wa  ACT bali nakataa wale wanaolazimisha watu waamini kuwa ACT ni  sehemu ya CCM. Yanaongelewa mengi kuwa Mhe.Zitto atafungwa mdomo kwa kupewa nafasi ya juu ili anyamaze, hayo ni  maneno ya chuki dhidi ya chama chetu kwani hata wao wanazitamani nafasi tulizozipata ACT katika kuilitumikia taifa  hili,” amesisitiza.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post