AKAMATWA AKIINGIZA SIMU GEREZA LA KEKO ZILIZOFICHWA NDANI YA NYAMA

Jeshi la Magereza jijini Dar es Salaam limefanikiwa kumkamata Ramadhan Nombo mkazi wa Mabibo alipotaka kula njama kuingiza simu katika Gereza la Keko lililopo wilayani Temeke.
Tukio la kijana huyo lilitokea juzi majira ya saa 11 jioni ambapo alimatwa baada ya mtambo wa ukaguzi kutoa ishara kwamba kuna hali ya tahadhari na walimkata akiwa na simu tano zilizowekwa ndani ya mapande ya nyama yaliyopikwa vizuri na kuchanganywa na viazi mbatata.
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, Augustine Mboje alisema kijana huyo mwenye wastani wa umri wa miaka 30 alikamatwa wakati akifanyiwa ukaguzi eneo la wageni ambalo hutumia kuingia gerezani hapo wanapowatembelea ndugu zao waliopo mahabusu.
Mkuu huyo alisema tukio hilo sio la kwanza kwani hutokea katika magaereza mbalimbali Dar es Salaam na kwamba mbinu mbalimbali hufanyika kutaka kuingiza simu gerezani lakini wamekuwa wakiwakamata.
Alisema kuwa baadhi ya watu hutumia ujanja wa kuficha simu kwenye mikate, ugali au wali lakini kutokana na ubora wa Askari na mitambo waliyonayo, wamekuwa wakifanikiwa kuwakamata.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post