ALICHOSEMA LOWASSA KUHUSU UTENDAJI KAZI WA RAIS MAGUFULI HADI SASA

Mjumbe wa Kamati Kuu wa CHADEMA na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Lowassa amesema kuwa Rais Dkt Magufuli alianza kwa kufanya kazi vizuri lakini licha ya kuwa amefanya baadhi nzuri, lakini bado kuna mengine mabaya aliyoyafanya.
Lowassa aliyasema hayo jana alipokuwa akifanya mahojiano na mtangazaji wa Azam Tv aliyetaka kujua hadi hapa tulipofikia, ni mambo gani anayoweza kusema kuwa Rais Magufuli amefanya vizuri na yeye anajivunia hilo.
Lowassa alisema hawezi kukataa kuwa kuna mambo mazuri yamefanyika hadi sasa lakini kuna mengine mabaya pia.
Hata Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, wakati unafagia uwanja, kuna wakati unaweza ukafagia shilingi katika ya uchafu, alisema Lowassa akijaribu kuelezea kauli yake kuwa wakati unafanya mambo mazuri, unaweza ukajikuta pia unafanya mengine mabaya.
Aidha, Lowassa aliwataka watanzania kutomhukumu Rais Magufuli sasa, bali wamuache na baada ya kipindi fulani ndipo wanaweza kufanya hivyo.
Itakumbukwa wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2015, Lowassa alikuwa ndiye mpinzani mkubwa wa Rais Magufuli katika uchaguzi ambapo alikuwa akipeperesha bendera ya CHADEMA na kuungwa mkono na vyama vinavyounda UKAWA.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

SHARE THIS

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post