ALICHOSEMA ZITTO KABWE BAADA YA KUKAMATWA VIGOGO WA ESCROW

Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amemsifu Rais Dkt Magufuli kwa jitihada zake za kupambana na rushwa ambapo amesema kwa muda wote, leo ameona kuwa vita ya ufisadi ina maana kubwa.
Zitto ameyasema hayo leo kupitia ukurasa wake wa Twitter ambao ameandika jumbe kadhaa kupongeza jitihada hizo za Rais Magufuli ambapo katika moja ya jumbe zake alisema kuwa, kukamatwa kwa watuhumiwa hao wa sakata la Tegeta Escrow ni moja ya hatua kubwa sana za Rais Magufuli dhidi ya rushwa.
Zitto alisema kuwa licha ya kuwa amekuwa akimpinga Rais Magufuli katika mambo mbalimbali na ataendelea kumpinga, lakini katika hili la kukamatwa kwa James Rugemarila na Harbinder Sethi anamuunga mkono na kumpongeza sana.
Hapa chini ni jumbe za Zitto alizoandika kupitia ukurasa wake wa Twitter;
Arrest of IPTL/PAP barons on  is the single most bold step by President Magufuli against corruption
I extend my genuine and honest congratulations to PCCB. Let justice be done. Let's bust the  ring
Leo ninaona vita dhidi ya ufisadi Ina maana kubwa. Kumkamata Harbinder Singh Seth na kumfikisha mahakamani ni hatua kubwa ya kupongezwa


Rais Magufuli nimekuwa nakupinga kwenye mambo mengi, na nitaendelea kukupinga, lakini kwenye hili la IPTL umetendea nchi haki. Hongera Sana
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post