ALIYEKUWA MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO AZUNGUMZIA UTEUZI WA ANNA MGHWIRA

Uteuzi wa Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Bibi Anna Elisha Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro umeendelea kuzua maswali mengi miongoni mwa makada wa vyama mbalimbali pamoja na wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini.
Baadhi ya wachambuzi wamesema kuwa uteuzi huo ni mbinu inayotumiwa na chama tawala kuvidhoofisha vyama vya upinzani nchini kwa sababu ukishateuliwa huwezi kushiriki katika ujenzi wa chama chako na badala yake utakuwa ukitekeleza ilani ya chama tawala.
Anna Mghwira aliteuliwa juzi akichukua nafasi ya Said Meck Sadick aliyeandika barua kwa Rais Magufuli akiomba kuachia madaraka kwa kile alichosema kasi ya sasa inahitaji watu wenye nguvu zaidi yake yeye.
Akizungumzia uteuzi huo wa Anna Mghwira, Said Meck Sadick alimpongeza sana na kusema yeye hana jambo la kuzungumza zaidi ya kumpongeza na kumtakia mafaniko katika kuutumikia umma wa watanzania.
“Namtakia mafanikio mema, mengine nitamweleza wakati wa kukabidhiana ofisi.” alisema kiongozi huyo aliyeachia ngazi. Aidha alieleza “Siku nikionana naye nitamweleza kuwa ushirikiano ni jambo la msingi wa watendaji atakaowakuta.”
Kwa upande wake Anna Mghwira ambaye yupo nje ya nchi akihudhuria kongamano la wanawake viongozi Afrika hajazungumza jambo lolote, lakini kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe alisema kuwa kiongozi huyo akirejea nchini watatolea uamuzi uteuzi huo, kwa sababu aliyeteuliwa ni kiongozi wa ngazi ya juu ya chama, hivyo inahitaji maamuzi ya Kamati Kuu.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post