ALIYEKUWA MSAIDIZI WA IGP SIMON SIRRO AONDOLEWA NA RAIS MAGUFULI KIMYA KIMYA

Kikao cha Makamanda Wakuu kutoka Makao Makuu ya Polisi, Makamanda wa Mikoa na Vikosi vya Tanzania Bara na Zanzibar na viongozi wote Wakuu wa Polisi wa Mkoa wa Dar es Salaam waliokutanakatika Bwalo la Maofisa Wakuu wa polisi lililopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam inaelezwa kuwa waliafikia kuondolewa kwa cheo cha msaidizi wa mkuu wa jeshi la polisi.
Chaeo hicho cha Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi (DIGP) ambacho hadi leo kilikuwa kikishikiliwa na Abdulrahman Omari Juma Kaniki imethibitika kuwa kimeondolewa rasmi baada ya aliyekuwa akishikilia cheo hicho kuteuliwa kuwa Balozi.
Uteuzi huo umetangazwa leo ambapo kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ilisomeka kuwa, “Rais Magufuli amemteua DIGP Abdulrahman Omari Juma Kaniki kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo DIGP Abdulrahman Omari Juma Kaniki alikuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi.”
Image result for Abdulrahman Kaniki
Aliyekuwa (DIGP) Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi Abdulrahman Kaniki
Sababu zinazodaiwa kupelekewa cheo hicho kuondolewa kuwa hakina tija katika jeshi hilo. Lakini pia ilielezwa kuwa cheo hiko hakipo katika muundo wa vyeo vya Jeshi la Polisi Nchini, au hata nchi za jirani.
Cheo cha Naibu Mkuu wa Jeshi kilianzishwa mwaka 2014 na Rais Dkt Jakaya Kikwete akiwa madarakani.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post