ANNA MGWHIRA AVULIWA UENYEKITI ACT

Leo Chama cha ACT Wazalendo kimemvua uongozi Mwenyekiti wa chama hicho, Anna Mgwhira baada ya kuapishwa na Rais Dkt. John Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Akizungumza na waandishi wa habari leo hii, Kaimu Kiongozi wa ACT Wazalendo, Samson Mwingamba alisema kamati ya uongozi wa ACT ulikutana leo kwa lengo la kujadili jinsi Mwenyekiti wao huyo atakavyoweza kutimiza kwa ufanisi majukumu ya nafasi hizo mbili alizokuwa nazo za Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Mwenyekiti wa Chama kwa wakati mmoja.
“Kama chama baada ya kutafakari kwa kina na baada ya mashauriano baina yake na viongozi kutumia katiba ya chama, anakoma kuwa kiongozi kwa kuwa kutakuwa na mgongano wa majukumu na maslahi hivyo anakoma kuwa Mwenyekiti,” alisema.
Kamati ya chama hicho imemchagua Yeremia Maganja kuwa Kaimu Mwenyekiti. Pia imempongeza Rais Magufuli kwa kumteua Mama Mgwhira. Pamoja na kusimamishwa Uenyekiti, Mama Mghwira bado anaendelea kuwa mwanachama halali wa chama hicho.
Uamuzi huo umefikiwa baada ya majadiliano ya Kamati ya uongozi wa Chama kwa kuzingatia ibara ya 17 ya katiba ya chama hicho ambayo inatamka kuwa kiongozi wa chama atakoma kuendelea na madaraka yake iwapo atashindwa kutekeleza majukumu yake.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post