ASKARI 6 WALIOMTOA MNYIKA NDANI YA UKUMBI WA BUNGE WAONDOLEWA BUNGENI

Spika wa Bunge, Job Ndugai (Mb) ameamuru Askari Polisi sita waliokuwa zamu kulinda ukumbi wa Bunge siku ya Ijumaa wahamishwe kituo cha kazi na kupelekwa wilayani.
Uamuzi huo wa Spika wa Bunge umekuja kufuatia kile alichodai kuwa Askari hao walishindwa kutekeleza sawasawa amri aliyotoa ya kumtoa nje ya ukumbi wa Bunge, Mbunge wa Kibamba (CHADEMA), John Mnyika.
Hatua ya Mbunge John Mnyika kutolewa nje ilifikiwa baada ya kukataa kukaa chini na kutulia kumpisha mbunge mwingine achangie kwa kila alichodai kuwa kuna mbunge mmoja alimuita yeye ni mwizi wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka 2017/18.
Habari za Askari hao kuhamishwa zilithibitishwa na Spika jana bungeni wakati wabunge wakichangia maoni kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhusu adhabu za wabunge wawili wa CHADEMA, Ester Bulaya na Halima Mdee.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alisema kuwa, kama Bunge haliwahitaji Askari hao, jeshi hilo linawahitaji na watapelekwa hatika wilaya nyingine.
Mbunge John Mnyika alifungiwa kuhudhuria vikao vya bunge kwa wiki moja ambapo adhabu hiyo inaisha Ijumaa Juni 9 mwaka huu.
Spika wa Bunge alisema Mnyika aliondolewa ndani ya ukumbi wa bunge kwa ubinadamu ambao haujawahi kutokea hadi yeye mwenyewe akawa anawashangaa wale askari na ndio sababu ameamua waondoke wote. Ndugai aliyasema hayo alipokuwa akipinga kauli iliyotolewa na Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea aliyesema kuwa Mbunge John Mnyika aliondolewa bungeni kama mwizi.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post