ASKOFU GWAJIMA ASEMA ANGEKUWA RAIS ANGEWACHUKULIA HATUA HII WACHUNGAJI WOTE

Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema kuwa kama angelikuwa Rais wa nchi angewaita wachungaji wote na kuwaambia waombe uchumi wa nchi ukue, na kama wangeshindwa basi angewafunga gerezani kwa muda wa miaka mitatu.
Askofu Gwajima ameyasema hayo leo Jumapili Juni 4 wakati akihubiri kanisani kwake  ambapo amesema haiwezekani kuwa na viongozi wengi wa kanisa wanaomba kila siku halafu nchi bado ipo kwenye hali mbaya.
Ukiona jamii imekumbwa na matatizo ujue kuna tatizo kwenye kanisa, ukiona viongozi hawaheshimu sheria ujue kuna tatizo kwenye kanisa, ukiona uchumi wa nchi haukai sawa ujue kuna tatizo kwenye kanisa, hivyo ningewakusanya wachungaji wote, wamuombe Mungu na wakishindwa ningewafunga miaka mitatu, najua huko gerezani wangekuwa wanaomba na mambo yangekuwa sawa.
Askofu Gwajima alikuwa akitolea mfano kwenye Biblia ambapo kipindi Israel inapitia kwenye njaa kali sana, Mfalme alikasirishwa na kuhoji wako wako wapi viongozi wa dini, na kwanini hawatabiri hali hii ibadilike?
Mfalme akasema kuwa, ikifika kesho saa nne asubuhi, hali haijabadilika, Mtumishi wa Mungu Elia akamatwe akatwe kichwa na kipelekwe kwake. Elia kusikia taarifa hizo alifunga, akaomba na keshi yake watu wakapata chakula.
Gwajima alisema viongozi wa dini siku hizi wamekuwa waongo, bila kuwatisha kidogo hawawezi kutabiri, hawawezi kuomba ili mataifa yaweze kuinuka.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post