ASLAY NDIYO CHANZO CHA YAMOTO BAND KUVUNJIKA

Baada ya watu wengi kujiuliza kwa muda mrefu kipi hasa kimepelekea kundi la Yamoto Band kusambaratika licha ya kuwa walikuwa wakifanya vizuri kwenye muziki, msanii mmoja aliyekuwa anaunda kundi hilo amefunguka na kueleza kuwa Aslay ndiye alikuwa chanzo cha wao kusambaratika.
Beka Flavour kutoka Yamoto Band amesema kuwa kundi hilo lilianza kuwa na mgogoro baada ya Aslay kutoa wimbo wa Kidawa bila kumshirikisha mtu yeyote, au hata viongozi wa kundi hilo.
Alipoulizwa sababu za kuchukua uamuzi huo, Aslay anadaiwa alisema kuwa alikuwa akijaribu tu ambapo wimbo huo kwa kiasi fulani ulipokelewa vizuri.
Beka Flavour ameyasema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio na kutanabaisha kuwa baada ya wao kuona Aslay ametoa wimbo wake mwenyewe na wao waliomba uongozi kutoa nyimbo zao wenyewe. Alisema waliona bora na wao watoe nyimbo zao wenyewe sababu kama wangesubiri wangonekana labda hawawezi kuimba wenyewe.
Tayari wasanii wa kundi hilo wameanza kufanya kazi mmoja mmoja huku Aslay akiwa ametoa nyimbo 4 hadi sasa.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post