BAADA YA ALI KIBA, DIAMOND KUGOMEA KUIMBA PAMOJA WIMBO WA SERENGETI BOYS, RAIS WA TFF AZUNGUMZA HAYA

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Jamal Malinzi amegoma kuwazungumzia wasanii wa Bongo Fleva, Ali Kiba na Diamond kuhusu majukumu ya soka waliyopewa na waziri.
Ikumbukwe kuwa wasanii hao waliteuliwa katika kamati maalum ya kuiunga mkono timu ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka Serengeti Boys na kuichangia licha ya kutolewa katika mashindano ya AFCON U-17 katika hatua ya makundi.
Baada ya kushukuru Watanzanzania na kueleza mipango yao kwa vijana wa Serengeti Boys, Malinzia liulizwa juu ya Diamond na Ali Kiba kutoonyesha uzalendo wa kukubali kuimba wimbo pamoja wa kuhamasisha.
Wawili hao waliteuliwa na Mbunge wa Mtama Nape Nnauye wakati akiwa Waziri wa Michezo aliunda kamati ya uhamasishaji kuhusiana na Serengeti Boys kushiriki AFCON miongoni mwa waliyokuwemo katika kamati hiyo ni Diamond na Ali Kiba.
“Naomba nisiongee chochote kuhusu Diamond na Ali Kiba naomba sana mimi nashukuru tu ni wenzetu walichaguliwa kuingia katika kamati ya uhamasishaji ya Serengeti Boys na aliyekuwa waziri husika, mheshimiwa Nape Nnauye, basi mimi niishie kuwashukuru tu.”
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post