BAADHI YA JAMII NCHINI HUTUMIA BANGI KAMA MBOGA YA MAJANI

Serikali imesema kuwa haitambua kama bangi ni moja ya mboga za majani na kuwa itawachukilia hatua kali watu wote au jamii za watu wanaotumia bangi kama mboga.
Naibu Waziri wa Afya, Hamis Kigwangalla aliyasema hayo jana bungeni wakati alipokuwa akijibu swali dogo la nyongeza la Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare (CHADEMA), aliyetaka kujua kama serikali inafahamu kuwa kuna baadhi ya makabila nchini ambayo kwa utamaduni wao, hutumia bangi kama mboga ya majani.
Nafahamu kuwa serikali inapinga matumizi ya bangi, lakini kwenye baadhi ya maeneo tumejulishwa kuwa, vijana baada ya kuvuta bangi wanafanyakazi kuliko uwezo wao wa kawaida. Je! Hufikiri kuwa uamuzi wa serikali kuzuia matumizi ya bangi yatakwamisha juhudi za kuelekea Tanzania ya viwanda kwa kupoteza nguvu kazi hiyo kwenye sekta muhimu kama ya kilimo? aliuliza mbunge huyo.
Akijibu swali hilo, Kigwangalla alisema kuwa matumizi ya bangi ya madhara ya kimwili na kiakili kwa binadamu. Baadhi ya madhara haya ni pamoja na ukichaa, magonjwa ya akili, kuharibu homoni za kike na za kiume na pia kuifanya mishipa ya ateri kuwa migumu.
Zaidi, Dk. Kigwangalla alisema kuwa bangi ina takribani kemikali hatarishi 113 ambapo kemikali ya hatari zaidi ni Tetrahydrocannibol (THC). Uvutaji wa bangi ni hatari sana hasa kwenye maeneo yenye watu wengi kwani humuathiri hata aliyekaa pembeni ambaye havuti kwa kuvuta moshi wa bangi bila kukusudia.
Aidha, Dk. Kigwangalla alisema kuwa serikali itaendelea na mpango wake wa kuwakamata wale wote wanaojihusisha kwa namna yoyote na bangi na watachukuliwa hatua stahiki.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post