BARUA YA MKURUGENZI MKUU WA ACACIA KWA WAFANYAKAZI WAKE

SHARE:

Jana (juzi) ilikuwa ni siku nyingine ngumu kwa kila muajiriwa wa Acacia au mtu yeyote anayefanya kazi au kuhusika kwa namna yoyote kwenye...

Jana (juzi) ilikuwa ni siku nyingine ngumu kwa kila muajiriwa wa Acacia au mtu yeyote anayefanya kazi au kuhusika kwa namna yoyote kwenye utendaji kazi wa migodi yetu. Ripoti za vyombo vya habari kwa wiki chache zijazo vitatuweka kwenye wakati mgumu sisi, familia zetu na marafiki zetu. Hali itakuwa ngumu zaidi kwa asilimia 96 ya wafanyakazi kwenye migodi yetu ambao ni Watanzania kwakuwa wananchi wenzenu wanafikiri kuwa mmekosa uzalendo na mmekuwa mkiwaibia kwa miaka mingi sasa na kufanya maisha yao kuwa duni.
Nataka kuweka wazi kuwa yale yaliyowasilishwa na kamati zote mbili zilizoundwa na Rais kimsingi hayana ukweli, tofauti na watu wengi wanavyosema na kuamini. Hatujawahi kukwepa kodi, hatujawahi kughushi nyaraka yoyote ili tujaribu kutolipa mrabaha na pia hatujawahi kufanya kazi kinyume na Sheria za nchi. Nitaelezea kwa nini tuhuma hizi zilizotolewa jana (juzi) ni za uongo na kwa nini kamati zimempatia Rais ripoti za upotoshaji kwa mara nyingine tena. Tunaendesha Acacia kama kampuni ya kimataifa, na tunategemea waajiriwa wote kuwa na kiwango cha juu kabisa cha uadilifu. Kwa lugha nyepesi kabisa, hiki tulichotuhumiwa kukifanya hakiwezekani.
Tuangalie zaidi maelezo haya: tunatuhumiwa kuwa tunaendesha shughuli zetu kinyume na Sheria za nchi kwa miaka 19 iliyopita kwa kuwa Acacia Mining plc haijasajiliwa nchini. Hatufanyi shughuli zetu kinyume na Sheria za nchi. Migodi yetu inamilikiwa na inafanya kazi kwakuwa imesajiliwa nchini Tanzania kwa mujibu wa matakwa ya Sheria. Kampuni hizi (Pangae Minerals Limited, Bulyanhulu Gold Mine Limited na North Mara Gold Mine Limited) zinalipa kodi zote stahiki na tunawasilisha taarifa zetu za fedha za kila mwaka kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania, TRA. Kampuni hizi zote kwa pamoja zinamilikiwa na Acacia Mining plc ambayo ndiyo inayomiliki kundi la makampuni yote yaliyomo ndani ya Acacia. Kwa sababu ya umiliki huu, Acacia ndio imebeba jina ikiwakilisha migodi yetu yote iliyopo Tanzania. Acacia ina kampuni nyingi duniani, na nchi za Afrika ambazo tuna miradi ni Kenya, Burkina Faso na Mali.
Acacia Mining plc ni kampuni iliyosajiliwa nchini Uingereza. Izingatiwe kuwa kwa miaka mingi sasa tumejaribu kuwaelezea TRA kuwa Acacia Mining plc ni kampuni ya Uingereza ambayo ipo kwenye masoko ya hisa ya jijini London na Dar es salaam na inamilikiwa na mamia ya wanahisa. Muundo huu wa kampuni upo sawasawa na miundo ya kampuni nyingi za kimataifa zinazofanya kazi nchini Tanzania na hatupo kinyume na Sheria wala hatuutumii kama njia ya kukwepa kodi kwa namna yoyote ile. Muundo huu wa kampuni pia sio siri yoyote (tumekuwa tukitoa taarifa kwa umma kila mwaka juu ya muundo wa kampuni yetu kwenye ripoti zetu za ukaguzi wa mahesabu na kwa TRA pamoja na Taasisi nyingine za Serikali. Pia hili tuliliweka kwenye taarifa zetu zilizopo kwenye Mamlaka ya Udhibiti wa Masoko ya Mitaji Tanzania (CMSA) wakati tunajiorodhesha kwa mara ya pili katika Soko la Hisa la Dar es salaam mwaka 2011.
Pia tunatuhumiwa kulipa kodi kidogo ambapo hadi sasa tunadaiwa Dola za Marekani bilioni 50 (Tsh. Trilioni 110). Hili si kweli. Tujadili kiwango hiki cha pesa kwanza. Kama kiwango hiki cha pesa kingekuwa sahihi, na kwa kutumia viwango vya kawaida vya kodi vya asilimia 30 kwenye mauzo tu (sio katika faida ambayo ndiyo inavyotakiwa kulipiwa kodi) inatakiwa kumaanisha kwamba tumefanya mauzo ya zaidi ya Dola za Marekani  bilioni 150 (Tsh. trilioni 33) kwa miaka 15 iliyopita.
Kampuni kubwa zaidi ya uchimbaji madini duniani, BHP, ina migodi ipatayo 20 kwenye nchi 10 ambayo ina thamani ya Dola za Marekani bilioni 90 (Tsh. trilioni 200). Kiasi hiki sisi hatuwezi kukifikia kwa migodi yetu mitatu tu. Thamani ya kampuni yetu yote kiujumla inakadiriwa kuwa ni Dola za Marekani bilioni 1.2 (Tsh. trilioni 2.6) lakini tunatakiwa kulipa malimbikizo ya kodi yanayofikia Dola za Marekani bilioni 50 (Tsh. trilioni 110). Jambo hili haliingii akilini.
Kiuhalisia, mapato tuliyotengeneza kwenye migodi ya Bulyanhulu ana Buzwagi tangu tumeanza uchimbaji si zaidi ya Dola za Marekani bilioni 6 (Tsh. trilioni 13.2) ambayo inajumuisha na mauzo ya vipande vya dhahabu. Kama ingekuwa ni mauzo ya mchanga wa madini pekee, basi ingekuwa ni  Dola za Marekani bilioni 3.3 (Tsh. trilioni 7.2) kwa karibu miaka yote 15. Kama mnavyoelewa, hii ni kampuni ambayo mahesabu yake yanakaguliwa na wakaguzi wa ndani na wa kimataifa (na makampuni yanayoongoza kwa ubora wa ukaguzi wa mahesabu duniani), tunauza bidhaa zetu kwa wafanyabiashara na wayeyushaji wanaotulipa pesa ambayo ni thamani ile ile ya mzigo tunaowapatia na tunayaelezea yote haya katika kila upande tuanofanya nao biashara. Tungewezaje kukwepa kulipa kodi ambayo ni zaidi ya mara 10 ya mauzo yetu? Kwa lugha rahisi kabisa hili lisingewezekana.
Sitapitia tuhuma zote kwenye tamko hili, lakini nataka ieleweke wazi kuwa, tumekuwa tunatoa taarifa kamili za madini tunayochimba na kuuza. Kwa mfano, hatujawahi kujaribu kudanganya idadi ya makontena ya mchanga tunavyouza. Jambo hili lisingewezekana kufanyika  hata kama tungetaka kudanganya kwa sababu ya idadi kubwa ya kampuni na mawakala wa serikali wanaohusika katika mchakato mzima kuanzia malori ya kubebea, bandarini, upakiaji na usafirishaji wa melini na mwisho kwa wachenjuaji tunaowauzia.
Jana (juzi) ilikuwa siku ya majonzi kwetu kwakuwa inahatarisha kabisa uwepo wa kampuni yetu. Taarifa ya kamati ya pili imeelekea kutumia mapendekezo yaliyotolewa na taarifa ya kamati ya kwanza ambayo zaidi ya mara moja tumesema kuwa haikuwa sahihi, badala ya kuchukua taarifa tulizokusanya kwa zaidi ya miaka 20, wameweka makadirio makubwa kupita kiasi ya kiasi cha madini ndani ya makontena. Tunapinga  taarifa iliyotolewa na kamati ya pili, kama tulivyoipinga taarifa ya kamati ya kwanza. Tuliomba tupatiwe ripoti ya kamati ya kwanza ili tuweze kuipitia na kuangalia jinsi walivyofikia kwenye hesabu hizo ambazo haziwezekani, lakini mpaka sasa hatujapatiwa ripoti hiyo. Pia tutaomba tupatiwe taarifa ya kamati ya pili, ili tuweze kuelewa ni jinsi gani walifikia majumuisho waliyoyawasilisha jana (juzi), na tunategemea Serikali itatupatia nakala ya ripoti hizo. Tuliomba iundwe tume huru ya kuchunguza kiasi cha madini kilichomo kwenye kamontena hayo ili kuepusha mgogoro kama huu uliotokea sasa wa kutuhumiwa mbele ya umma juu ya wizi ambao kimsingi haujawahi kufanyika lakini kwa bahati mbaya sana mpaka sasa hatujapewa idhini katika hilo.
Kutokana na jinsi tukio la jana lilivyokuwa linaendelea na vyombo vya habari vinavyoripoti, ni wazi kuwa tunaonekana kama si wazalendo na kwamba tunaiba madini ya Tanzania na tuna mikataba ya kinyonyaji. Hili halikaribii ukweli hata kidogo; sisi ni viongozi wa sekta ya uchimbaji madini Tanzania. Kwa miaka mingi sasa tumefanya mapendekezo sisi wenyewe juu ya kurekebishwa baadhi ya vipengele vya mikataba iliyosainiwa miaka mingi iliyopita ili kuhakikisha faida kubwa zaidi inabaki Tanzania, hata kabla ya wawekezaji waliotoa pesa kujengwa kwa mitambo hii na pia kabla ya pesa waliyoiwekeza haijarudi. Tunalipa kodi hata kabla ya kufanya biashara, ongezeko la kiwango cha mrabaha, ongezeko la tozo za serikali za maeneo iliyopo migodi na tunawekeza zaidi kwenye jamii zinazotuzunguka ukilinganisha na kampuni zote zinazoendesha shughuli za uchimbaji wa madini zikiwekwa pamoja. Tuna Watanzania wengi zaidi kwenye nafasi za uongozi kwenye kampuni zetu na zaidi ya asilimia 96 ya wafanyakazi wetu wote ni Watanzania. Kila mmoja kati ya watu hao tumempatia mafunzo ya hali ya juu na kumuendeleza kwa miaka mingi na tumekuza baadhi ya vipaji vinavyoongoza hapa nchini.
Kwa ilivyo sasa, taarifa ambayo si sahihi na yasiyowezekana kutokana na kuchunguza sehemu tu ya makontena 44 pekee kati ya makumi ya maelfu ya makontena sasa inatumika kuharibu sifa nzuri tuliyoijenga kwa miaka mingi ya kuwa muwekezaji mkubwa zaidi wa nje hapa nchini, moja kati ya waajiri binafsi wakubwa zaidi na moja kati ya walipa kodi wakubwa zaidi nchini. Tumewekeza zaidi ya Dola za Marekani bilioni 4 (Tsh. trilioni 8.8) hapa nchini kujenga na kuendesha migodi hii, tumetumia zaidi ya Dola za Marekani bilioni 3 (Tsh. trilioni 6.6) kwa wasambazaji Watanzania kusaidia kuendesha biashara yetu na kulipa zaidi ya Dola bilioni 1 billion (Tsh. trilioni 2.2) kama kodi na mrabaha Serikalini. Sisi ni wadau wa muda mrefu wa maendeleo wa Tanzania ambao toka mwanzo tumekuwa tukifanya kazi kwa mujibu wa Sheria. Tunaamini kuwa tuna nafasi muhimu ya kufanya kazi na serikali kufanikisha malengo ya kuisaidia Tanzania kufikia malengo yake ya maendeleo. Tutaendelea kutafuta muafaka kwa njia ya majadiliano na serikali. Kama hili litashindikana basi itakuwa ni dalili mbaya sana kwa wawekezaji wote waliopo nchini sasa na waliotarajia kuja kuwekeza nchini. Naamini ukweli utajulikana na nitaendelea kufanya kila lililo ndani ya uwezo wangu kulifanikisha hilo. Mpaka itakapofika muda huo, tafadhali endeleeni kuwa imara na salama, na nasikitika sana mmejikuta mpo ndani ya sakata hili.
Mkurugenzi Mkuu
Acacia

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: BARUA YA MKURUGENZI MKUU WA ACACIA KWA WAFANYAKAZI WAKE
BARUA YA MKURUGENZI MKUU WA ACACIA KWA WAFANYAKAZI WAKE
https://4.bp.blogspot.com/-xSeGf4dG2rI/WUIqn12LsCI/AAAAAAAAcWc/vhMhl9wp47w8vjVWcn0gk-Ta5fgocwTXwCLcBGAs/s1600/xhg-750x375.jpg.pagespeed.ic.MAPwcZ4-xm.webp
https://4.bp.blogspot.com/-xSeGf4dG2rI/WUIqn12LsCI/AAAAAAAAcWc/vhMhl9wp47w8vjVWcn0gk-Ta5fgocwTXwCLcBGAs/s72-c/xhg-750x375.jpg.pagespeed.ic.MAPwcZ4-xm.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/06/barua-ya-mkurugenzi-mkuu-wa-acacia-kwa.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/06/barua-ya-mkurugenzi-mkuu-wa-acacia-kwa.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy