BREAKING: ADHABU ILIYOTOLEWA NA BUNGE KWA WABUNGE HALIMA MDEE NA ESTHER BULAYA

Wabunge wa CHADEMA, Halima James Mdee (Kawe) na Esther Bulaya (Bunda Mjini) wameadhibiwa kwa kutoruhusiwa kuhudhuria vikao vya bunge vilivyosalia hadi mkutano ujao wa bunge la bajeti mwaka 2018/19.
Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imesema kuwa wabunge hao wamemaliza adhabu ndogo zilizopo kwenye kanuni za makosa za Bunge.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, George Mkuchika aliliomba bunge kujadili adhabu kwa wabunge hao ambapo hukumu hiyo iliungwa mkono na wabunge walio wengi.
Wabunge hao walifanya makosa siku ya Ijumaa wakati Mbunge wa Kibamba, John Mnyika alipokuwa akitolewa nje ya ukumbi wa Bunge na Askari, ambapo Halima Mdee alikuwa akiwazuia Askari kumtoa huku, Bulaya akiwataka wabunge wengine wa CHADEMA watoke nje.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post