CHANZO HALISI CHA UGOMVI WA ALIKIBA NA DIAMOND CHAWEKWA HADHARANI LEO

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, AT amesema ugomvi wa Diamond OPlatnumz na Alikiba ulianzia nchini Oman ambapo walienda kufanya matamasha ya muziki.
AT ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza katika kipindi cha XXL cha Clouds FM, ambapo alifafanua kuwa mashabiki wengi wa muziki nchini hawajui mwanzo wa mvutano wa wawili hao ila wao wenyewe ndio wanajua ukweli huo.
“Tulikuwepo tupo Oman kwenye hoteli moja inaitwa Dream tulikuwa tuna ‘show’, kwa hiyo walikuwa wanacheza game, Alikiba amechagua Real Madrid na Diamond Barcelona, mimi nimekaa pembeni naangali watu wanacheza game yao. Ali akawa amefungwa mbili, akawa anataka kupiga free kiki kwenye game Diamond akamsukuma akamwambia halafu mwanangu nakutafuta siku nyingi,” amesema AT. Alikiba akanyanyuka ikabidi na mimi ninyanyuke sasa, nikamuuliza Ali tatizo nini mbona kama mnataka kupigana halafu tupo ugenini wazee vipi?  Akaniambia huyo dogo kuna vitu anavifanya mimi sijavipenda,” ameongeza.
AT aliendekea kusema kuwa, “Mwisho wa siku naona kama vile vitu vinaendelea halafu watu wanakurupuka wala tatizo wao hawalijui. Ebu watafute ukweli ulipo, sijui huyo kamtoa kwenye wimbo huyo, kuna jambo lingine ambalo lipo. Kiukweli kuna vitu ambavyo pengine wao wenyewe wanavijua ni vikubwa zaidi,” amesisitiza.
Mwanamuziki huyo alisema kuwa alifanikiwa kuwazuia mafahali hao wawili kupigana ugenini kwa sababu kama sio yeye basi mmoja angekuwa hana meno.
Aidha, AT alisema kuwa yeye ni shabiki wa Alikiba laki haimaanishi kuwa anamchukia Diamond Platnumz.
“Mimi ni shabiki mkubwa wa AliKiba lakini napenda sana kusikiliza nyimbo za Diamond Platnumz sina tatizo naye. Mimi ni shabiki namba 1 wa Alalikiba kuliko hata Abdu Kiba. Ila sio kwamba namchukia.”
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post