“DIAMOND HAKUNILIPA,” – SAIDA KAROLI

Mwanamuziki Saida Karoli amesema hajawahi kupokea fedha yoyote kutoka kwa wasanii waliorudia ama kutumia vionjo vya wimbo wake Maria Salome (Chambua kama Karanga) tofauti na inavyodhaniwa na wengi.
Saida ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wa ‘Orugambo,’ huku akiwa mbioni kukamilisha albamu yake yenye nyimbo 17 anasema kuwa alimpa Diamond ruhusa ya kurudia wimbo huo kwakuwa aliamini ungemrudishia umaarufu wake na amefanikiwa, lakini hajawahi kupokea fedha yoyote kutoka kwa Diamond wala msanii mwingine yeyote aliyerudia au kutumia vionjo vya wimbo huo.
“Mimi sikupokea fedha yoyote kutoka kwa Diamond. Mimi nilimpa ule wimbo ili autumie kwa kuwa nilishafeli kwenye muziki, nikaona nikimnyima na mimi nilikuwa nimeshuka kisanii haitapendeza. Nikaamua kumpa ili autumie labda utanitambulisha tena kwenye tasnia hiyo, kwahiyo hatukuwa na makubaliano ya kunilipa fedha kama ilivyokuwa ikivumishwa.”
“Pia, nia yangu kubwa haikuwa kupata fedha kwa kurudia wimbo huo, ila nilijua wimbo huo ukiimbwa na Diamond utapata nafasi kubwa, na mimi umenirudisha. Nashukuru na naamini nilipokosea sitarudia tena makosa ya kipindi hicho,” alisema Saida.
HT @ MTANZANIA
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post