FAHAMU JINSI YA KUTAMBUA UWEZO WA SPIDI YA MATAIRI YA GARI LAKO

Katika makala iliyopita tulichambua na kukuelezea namna ya kujua tairi la gari limetengenezwa muda gani na pia tulitoa ushauri juu ya matumizi ya tairi za gari ili kukuepusha wewe kupata ajali zinazoepukika. Kama kwa sababu moja au nyingine hukuweza kusoma makala hiyo, unaweza kuisoma sasa kwa kubofya kiungio (link) iliyopo hapa chini ili uweze kufuatilia mtiririko huu.
Kikubwa tutakachozungumzia leo ni jinsi ya kutambua uwezo wa kasi/spidi ya tairi yako unayotumia ili usiende spidi zaidi ya hiyo na kusababisha tairi ya gari lako kupasuka na hata kupelekea kifo.
Mara kadhaa tumeshuhudia watu wakifariki dunia baada ya matairi ya magari yao kupasuka ambapo suala la spidi ya gari na uwezo wa tairi hutofautiana na tairi hupasuka.
Kila tairi inauwezo wake wa spidi ambapo pembeni ya tairi hiyo kuna maelezo yanayoonyesha uwezo huo. Uwezo wa spidi ya tairi huonyeshwa na uwepo wa herufi kama vile, M, N, P, Q, R, S, T, U, H, V, W, au Y. Kila moja ya herufi hizi huwakilisha uwezo fulani cha spidi ambyo tairi yako inaweza kwenda kwa kipindi fulani.

Mfano, kama tairi ya gari lako imewekwa alama ‘H’, hii inaama kuwa unauwezo wa kwenda hadi spidi ya 130 mph (209 kmh). Je! Nikiendesha gari zaidi ya kiwango kilichoonyeshwa kwenye tairi litapasuka? Jibu ni kuwa, halitapasuka kwa wakati huo huo, ila ukiendesha kwa umbali mrefu kiasi, litakuwa kwenye hatari kubwa ya kupasuka kwa sababu huo si uwezo wake.
Image result for determine tire speed rating
Unapobadilisha tairi ya gari, hakikisha kuwa tairi unayoiweka inaendana na uwezo wa spidi wa tairi nyingine zilizopo, lakini pia unashauri kuwasiliana na wataalamu kama kuna tatizo katika mfumo wa matairi wa gari lako.
Kuepuka kupunguza mwendokasi wa gari lako, hakikisha kuwa tairi zinalingana uwezo wa spidi au uweke tairi ambayo inaspidi kubwa kuliko nyingine. Ukiweka tairi ambayo ina uwezo mdogo kuliko matairi mengine yaliyopo, itapunguza uwezo wa gari lako kwenda kasi lakini pia ni hatari kwa usalama wako.
Hapa chini ni viwango mbalimbali vya spidi za matairi;
 • M= 81 mph
 • N= 87 mph
 • P= 93 mph
 • Q= 99 mph
 • R= 106 mph
 • S = 112 mph
 • T = 118 mph
 • U = 124 mph
 • H = 130 mph
 • V = 149 mph
 • W = 168 mph***
 • Y = 186 mph***
 • ZR = zaidi ya 149 mph**
Tairi ya gari yoyote yenye uwezo wa kwende spidi zaidi ya 149mph, kwa upendeleo wa mtengenezaji anaweza akatumia herufi ‘Z’ wakati anapotengeneza matairi hayo, mfano (245/40ZR18). Kwa mfano huo tuliouonyesha hapo ambao una herufi ‘ZR’ inamaanisha kuwa tairi hiyo inauwezo wa kwenda zaidi ya 149 mph.

Muhimu, kama maelezo ya kwenye tairi yamewekwa (ZR) bila kuwapo kiwango kingine kinachoonyesha uwezo wa tairi, inamaanisha tairi hiyo unaweza kwenda zaidi ya 149 mph, mfano (245/40ZR18). Katika mfano huo kuna ‘ZR’ peke yake, hakuna herufi nyingine inayoonyesha uwezo wa spidi ya tairi. Kinyume chake ni kuwa, kama kwenye maelezo ya tairi kuna ‘ZR’ lakini pia kuna herufi nyingine, mfano P235/45ZR17 97W, uwezo wa hiyo tairi ni ‘W’ ambayo inawakiliwa 168 mph. Hapa hatuangalii tena ile ‘ZR’ kwa sababu tayari uwezo wa tairi umewekwa.
Aidha, unashauriwa kuwa makini katika uwezo wa tairi ya gari lako kwani magari haya hujaribiwa katika maabara maalum ambazo mara nyingi hazifanani na maeneo halisi ambapo tairi zinakuja kutumika. Hali ya hewa, uimara wa gari, mgizo, namna ya uendeshaji wa gari, aina ya barabara, vyote hivi vinaathiri uwezo wa tairi.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post