HARMONIZE AMWEKA HADHARANI MPENZI WAKE MPYA NA KUSEMA YEYE BABA KIJACHO

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka lebo ya muziki ya WCB, Hamornize leo amkata mzizi wa fitina baada ya kuweka mambo hadharani na kusema kuwa mpenzi wake mpya ni mjamzito hivyo karibu atajifungua.
Msanii huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameweka picha ya Ultrasound ikionyesha kichanga kikiwa tumboni na kusema kuwa mchanganyiko wa kimakonde na mtoto wa kizungu hajui kitatoka kitu gani.
Haya yamekuja ikiwa ni siku chache tu tangu kijana huyo anayetamba na nyimbo kama Show Me, Nambie, Birthday alipoachana na aliyekuwa mpenzi wake, Jackline Wolper.
Lakini mbali na hiyo, alianza kwa kuweka picha ya mrembo mwenye asili ya magharabi na kuandika chini Ujinga ni wakati wa kwenda tu, huku akiongezea na mabusu kibao. Kwa hapo mtu mzima unaunganisha nukta halafu unapata mchoro kamili.
Huu ndio ujumbe alionadika Harmonize kuonyesha sasa na yeye anajiunga kwenye chama cha kuacha kodi ya meza;

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post