HIVI NDIVYO AMBAVYO JOHN BOCCO AMEKARIBISHWA SIMBA

Hatimaye Klabu ya Simba imefunguka kuwa mshambuliaji John Raphael Bocco amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Simba, baada ya kumalizana na timu aliyoichezea kwa misimu 10 mfululizo Azam FC.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe alithibitisha hilo siku kadhaa zilizopita na sasa klabu hiyo imemtambulisha mchezaji huyo leo kwa kumkabidhi jezi ya Simba.

Picha hiyo ya Bocco akikabidhiwa jezi ya Simba na rais wa klabu hiyo Evans Aveva, imeteka vichwa vya habari vya mitandao mbalimbali ambapo mashabiki wa Simba wameonyesha kufurahishwa na usajili huyo kutokana na tatizo la usahmbuliaji lililokuwa likiwasumbua msimu ulipita wa 2016/17.

Akizungumzia juu ya usajili huo Hans Poppe alisema: “Ni kweli Bocco tumemalizana naye baada ya kumpa mkataba wa miaka miwili ni mchezaji mzuri ambaye hata kocha Joseph Omog ameridhishwa na usajili wake.” 
Bocco alitaka dau la Sh milioni 40 kusaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kucheza Azam FC kwa mshahara ule ule wa Sh milioni 4.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post