IJUE HUDUMA YA KUJIUA KWA MSAADA WA DAKTARI

Mwaka 2014, Brittany Maynard alikuwa ni dada mwenye nguvu wa umri wa miaka 29 aliyekuwa anataka kuanzisha familia na mumewe ambao hawakuwa na muda mrefu toka wafunge ndoa wakati maumivu makali ya kichwa yalipoanza kumsumbua.
Matokeo ya uchunguzi: Kansa ya ubongo. Japokuwa amefanyiwa upasuaji mara mbili kujaribu kupunguza kasi ya ukuaji wa uvimbe huo, lakini ulirudi kwa kasi kubwa zaidi na mara moja akaambiwa amebakiza muda wa miezi sita tu wa kuishi. Akiwa anatakiwa kufanyiwa tiba ya kupigwa mionzi kabika ubongo wote ambayo pia isingeweza kumtibu ugonjwa huo, lakini ingesababisha kuchomamwa ngozi ya kichwa ambayo pia ingesababisha maumivu sugu yasiyoweza kupona kwa dawa ya morphine, mabadiliko ya umbo lake pamoja na kupoteza kumbukumbu, aliamua kujiua kwa msaada wa madaktari (medically assisted suicide).
Kufanikisha kifo hiki alichokiomba, ilimlazimu Brittany kuhama toka California kwenda Oregon, moja ya miji michache duniani inayoruhusu madaktari kuwasaidia wagonjwa wanaotaka kujiua. Katika wiki zake za mwisho maishani mwake, Brittany alitengeneza video ya dakika sita iliyohusu “kufa kwa heshima” ambayo iliibua hisia kali sana nchini Marekani. Alikufa kama alivyotaka, baada ya kunywa sumu ya dawa zinazoleta usingizi na kuzuia mfumo wa upumuaji alizopewa na daktari wake siku ya Novemba 1, 2014. Kabla haujatimia mwaka mmoja toka kifo chake, ikiwa ni shukrani za kipekee kwa video yake, jiji lake la California lilipitisha sheria ya msaada wa kujiua. Kwa kuongezea, sheria ya “kufa kwa heshima” ilipitishwa katika zaidi ya majiji yote nchini Marekani.
Kujiua kwa msaada wa madaktari kimsingi inamaanisha kuwa daktari anamuandikia mgonjwa dawa ambazo ni sumu ambazo mgonjwa atazimeza yeye mwenyewe. Hii ni tofauti na njia ya Euthanasia, ambapo daktari humlisha mgonjwa dawa hizi za sumu au kumchoma sindano.
Dhana hii ya kujiua kwa kusaidiwa na daktari si mpya. Imekuwa ikitumika toka kale na imekuwa ikaitwa majina tofauti.
Hata hivyo, pamoja na kutumika muda mrefu sana, imejipatia umaarufu zaidi katika kipindi cha hivi karibuni. Mwaka 1940 nchi ya Uswisi iliruhusu kujiua kwa njia hii na ikapita miaka mingi bila kuruhusiwa sehemu nyingine. Mwaka 1997 Colombia pia ikaruhusu aina hii ya kujiua ikifuatiwa na Uholanzi na Ubelgiji mwaka 2002, Luxembourg mwaka 2009, Uingereza na visiwa vya Wales mwaka 2010 na Canada mwaka 2016.
Hata hivyo, pamoja na kutumika sehemu nyingi, kumekuwa na ugumu hasa linapoibuka la kuruhusu jambo hili kisheria moja kwa moja — kwa woga kwamba wengi wataitumia pasipo kuwa na ulazima wowote.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post