KABURI LA ALIYEKUWA MUME WA ZARI, IVAN SEMWANGA KUFUKULIWA

Vyombo vya habari nchini Uganda vimeripoti kuwa mwanasheria mmoja ameiomba mahakama itoe ruhusa ya kufukuliwa kwa kaburi la aliyekuwa mfanyabaishara maarufu kutoka Uganda akiishi Afrika Kusini, Ivan Semwanga.
Bilionea huyo ambaye pia alikuwa mume wa Zari The Boss Lady alizikwa na kiasi kikubwa cha fedha kilichomwagwa kwenye kaburi lake na waliokuwa rafiki zake wanaofahamika kama ‘Rich Gang.’
Mwanasheria, Tugume Gideon ameiomba Mahakama Kuu ya Uganda kutoa kibali hicho ili fedha hizo ziweze kutolewa kaburini, kwani ni kinyume na sheria kufukia fedha ardhini ambazo ni moja ya nyara za serikali.
Ivan Semwanga alizikwa siku ya Jumanne Mei 30 nyumbani kwake Kayunga nchini Uganda.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post