KAMANDA SIRRO APOKEWA NA MAUAJI MENGINE KIBITI

Mara baada ya kuapishwa kwa Kamanda Sirro kuwa Inspekta Jenerali wa Polisi, wazee wa wilaya tatu za mkoani Pwani zilizokumbwa na matukio ya mfululizo ya mauaji ya kutumia silaha, Kibiti, Ikwiriri na Mkuranga waliomba wakutane na kiongozi huyo wa juu kabisa wa Jeshi la Polisi nchini ili kubaini chanzo na mbinu sahihi za kukomesha matukio hayo.
Ikiwa ni saa chache kabla ya kuanza kwa mkutano huo, watu wasiojulikana juzi usiku waliua kwa kumpiga risasi mkazi wa Ikwiriri ambaye alikuwa ni askari mgambo, Bwana Erick Mwarabu, nyumbani kwake Kazamoyo wilayani Rufiji.
Mganga Mkuu wa kituo cha afya cha Ikwiriri, Iddy Malinda alisema kuwa mwili wa marehemu Mwarabu akisema kuwa “Mawili yalikuwa mbavuni upande wa kulia na moja kichwani. Katika jeraha la kichwani, Mwarabu alipigwa risasi upande wa kushoto.”
Kwa mujibu wa majirani, watu hao walivunja mlango wa nyumba ya marehemu usiku na kufanya mauaji hayo kwa kumpiga risasi tatu na kutoweka bila kuchukua kitu chochote.
Mkuu wa wilaya ya Kibiti, Gullamhussein Kifu alisema kuwa tangu Aprili 30 mwaka jana hadi sasa, watu 18 wakiwamo viongozi wa serikali za vijiji wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana. Kifu alisema miongoni mwa watu hao wamo viongozi wa vijiji, vitongoji, wanachama wa CCM na askari tisa. Alikuwa akitoa ripoti hiyo katika ufunguzi wa mkutano huo kati ya wazee wa wilaya hizo na IGP Simon Sirro.
Akitoa taarifa kuhusu mkutano huo, Kamanda Sirro alisema kuwa watu wanaoendesha mauaji hayo wapo mbioni kukamatwa na kwamba siku zao zinahesabika akitahadharisha kuwa ubaya utalipwa kwa ubaya tu.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post