KAULI YA MAKAMU WA RAIS KUHUSU MIMBA KWA WANAFUNZI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewaonya wazazi ambao wamekuwa wakiwatetea wale wanaowapa mimba watoto wa kike na kusema kuwa serikali imejipanga kukabiliana nao vilivyo.
Makamu wa Rais amesema yeyote atakaye kamatwa na kuthibitika kuwa amempa mimba mtoto, hatokuwa salama kwani wamekuwa wakikwamisha wanafunzi kuendelea na masomo.
Aidha Makamu wa Rais amewaonya wazazi ambao hukaa vikao vya kimila na kumalizana kienyeji kati ya familia ya binti na ya mwanaume ambaye anakuwa amempa mimba, akisema jambo hilo halikubaliwi huku akiwaagiza viongozi wa serikali kushughulikia tatizo hilo.
Kauli hii ya Makamu wa Rais imekuja wakati maeneo mengi nchini yametawaliwa na mjadala kuhusu ama wanafunzi wanaojifungua waruhusiwe kurudi shule au wasiruhusiwe.
Mjadala huu umepamba moto baada ya tamko la Rais Magufuli alilotoa jana kuwa, chini ya utawala wake, hakuna mtoto ambaye atapata mimba aruhusiwe kuendelea na masomo kwani kwa kufanya hivyo ni kama kushawishi wanafunzi zaidi kuzaa angali wakiwa shule.
Kwa upande wake kambi ya upinzani bungeni, wamepinga kauli hiyo ya Rais wakisema kuwa tayari Wizara ya Elimu chini ya Prof. Ndalichako walishafanya uchunguzi kuhusu tatizo hilo na walikuwa tayari kuwaruhusu wanafunzi watakaojifungua kuendelea na masomo. Pia wameikosoa serikali na kusema haina kauli moja kwani kauli za Rais, Waziri wa Afya, Makamu wa Rais zinapishana.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post